Home Simba SC AFISA HABARI MPYA SIMBA ‘AMKATAA MANARA KIAINA’

AFISA HABARI MPYA SIMBA ‘AMKATAA MANARA KIAINA’


SIKU moja baada ya kuteuliwa na uongozi wa Simba kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ezekiel Kamwaga amesema kuwa asifananishwe na msemaji aliyeondoka klabuni Haji Manara katika utendaji wa majukumu katika timu hiyo.

Kamwaga alisema kuwa anatambua mchango mkubwa uliofanywa na Haji Manara katika timu hiyo hivyo hapaswi kulinganishwa nae kwa kuwa kila mmoja anasifa tofauti na mwenzake

“Manara amekuwa ni mtu muhimu katika timu yetu hivyo tunapaswa kumuheshimu kwa mchango wake mkubwa alioutoa na kuacha maisha mengine yaendelee” alisema.

Aidha Kamwaga alisema kuwa anaupongeza uongozi wa timu kwa kumpa nafasi hiyo na kuahidi kwenda na kasi ya mabadiliko ya timu hiyo kwenye uendeshaji.

“Nawashukuru bodi ya wakurugenzi kwa kuniamini kunipa tena nafasi hii, nawaahidi mashabiki wa Simba kufanya kazi kwa bidii na kuendana na mabadiliko ya kiutendaji y klabu yetu” alisema.

Kamwaga anachukua nafasi hiyo kwa miezi miwili baada ya Haji Manara kuamua kuacha majukumu ya kuendelea kuwa msemaji wa klabu hiyo.

SOMA NA HII  KAMA ULIDHANI MALENGO YA SIMBA NI MENGINE....HESABU HAYA KWA SASA.....