Home Uncategorized TANZANITE KUREJEA LEO BONGO NA KOMBE LAO LA COSAFA

TANZANITE KUREJEA LEO BONGO NA KOMBE LAO LA COSAFA


Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Miaka 20 ‘Tanzanite’ ilialikwa kushiriki michuano ya COSAFA iliyokamilika jana nchini Afrika Kusini na wameibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Inatarajiwa kuerjea leo nchini Tanzania pamoja na msafara wa viongozi ambao walikwea pipa kuipa sapoti timu hiyo.

Tanzanite mchezo wa mwisho walicheza na Zambia na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa kombe hilo.

Kocha Mkuu wa Tanzanite, Bakari Shime amesema kuwa ni zawadi kwa mashabiki wa Tanzania ambao wanapenda mpira na wanatoa sapoti kwa timu zote Tanzania.

SOMA NA HII  HATIHATI YA MECHI KATI YA SIMBA NA ALLIANCE KUFANYIKA LEO CCM KIRUMBA