Home Uncategorized FAINALI YA KUNDI LA TANZANIA AFCON ITANOGA KINOMA

FAINALI YA KUNDI LA TANZANIA AFCON ITANOGA KINOMA



KOCHA Mkuu wa Senegal, Aliou Cisse amesema kuwa mchezo wa fainali hautakuwa mwepesi kutokana na timu zote kuwa vizuri.

Senegal imetinga hatua ya fainali kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri kwa ushindi wa bao 1-0 la kujifunga kupitia kwa Dylan Bronn dakika ya 100 baada ya dakika 90 kukamilika bila kufungana.

“Utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia ni timu ambayo tulikuwa nayo kundi moja hivyo kila mmoja amejipanga kuibuka na ushindi tutapambana,” amesema.

Djamel Belmadi kocha wa Algeria ambaye timu yake imetinga fainali baada ya kuibamiza Nigeria mabao 2-1 amesema kuwa malengo ya timu ni kupata ushindi na wanaamini watacheza na moja ya timu bora.

“Mchezo hautakuwa mwepesi ila tunawaheshimu wapinzani wetu tunafurahi kutinga hatua ya fainali kwetu ni jambo la furaha,” amesema.

Timu zote zilizotinga hatua ya fainali zilikuwa kundi C ambalo lilikuwa na timu mbili za Afrika mashariki ambazo ni Kenya na Tanzania, walipokutana kwenye hatua ya makundi Algeria alimbamiza Senegal kwa bao 1-0.
SOMA NA HII  LIONEL MESSI ALIA NA WAAMUZI