Home Uncategorized ZAHERA WA YANGA KUSHUSHA JEMBE MOJA LA KAZI

ZAHERA WA YANGA KUSHUSHA JEMBE MOJA LA KAZI

MWINYI Zahera Kocha Mkuu wa Yanga, leo ameanza rasmi kukinoa kikosi chake ambacho kimeweka kambi mkoani Morogoro.

Zahera amesema kuwa kwa sasa anasubiri nyota wake mmoja ili afunge jumla mahesabu ya usajili.

“Malengo makubwa ya kwenye usajili kwa kisasi kikubwa yamekamilika, kwa sasa kuna nafasi moja tu ya mchezaji kwa nafasi ya ushambuliaji kisha baada ya hapo tunafunga hesabu jumla,” amesema Zahera. 

Dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi Daraja la kwanza linafugwa kesho Julai 31.

SOMA NA HII  BALE KUKIWASHA LEO SPURS