Home Simba SC MFARANSA WA SIMBA ANAIPIGA HESABU KUISHUSHA YANGA

MFARANSA WA SIMBA ANAIPIGA HESABU KUISHUSHA YANGA


 KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes raia wa Ufaransa, amesema kwamba, anataka kuitumia mechi yao ya leo Jumatano dhidi ya Prisons kwa ajili ya kuwasogelea wapinzani wake, Yanga.

 

Mfaransa huyo ameongeza kwamba, mechi hiyo pia ataitumia kwa ajili ya kuongeza presha kwa wapinzani wake Yanga ambao ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara hadi sasa.

 

Simba, Machi 10 watakuwa wenyeji wa Prisons katika mechi ya ligi kuu ambayo itapigwa Uwanja wa Mkapa, Dar. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa, Prisons waliibuka na ushindi wa bao 1-0.


Hivyo leo unatarajiwa kuwa mchezo wenye ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu muhimu.


Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 45 imecheza jumla ya mechi  19 inakutana na Tanzania Prisons ambayo ipo nafasi ya 10 na pointi 27.


Gomes amesema:-“Kwa sasa akili yetu ni juu ya mechi dhidi ya Prisons, hii ni muhimu kwetu kwa sababu tunataka kuwapa presha Yanga ambao wapo juu yetu.

 

“Tukishinda tutakuwa karibu yao zaidi na hii itakuwa nzuri kwetu, muhimu tutacheza tukiwa tunajua ni kitu gani ambacho tutakuwa tunakitaka,” alimaliza Gomes.

 

Yanga baada ya kucheza mechi 23 wapo nafasi ya kwanza Yanga wamekusanya jumla ya pointi 50.

SOMA NA HII  SIMBA KUTEKETEZA ZAIDI YA MILIONI 200 HUKO MOROCCO, MCHANGANUO UKO HIVI...