Home Habari za michezo SIMBA, INONGA MAMBO YAWA SHARI….YANGA WATAJWA KUUCHEZA MCHEZO KIMYA KIMYA….

SIMBA, INONGA MAMBO YAWA SHARI….YANGA WATAJWA KUUCHEZA MCHEZO KIMYA KIMYA….

Habari za Simba leo

Klabu ya Simba imemruhusu beki Henock Inonga Baka kisafiri kwenda kushughulikia masuala ya kifamilia, hata hivyo imemgomea mchezaji huyo ombi la kutaka kuvunja mkataba wake kienyeji

Inonga ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba aliomba alipe gharama ya kuvunja mkataba huo ili akatafute changamoto sehemu nyingine

Simba imemtaka awasilishe ofa ya timu inayotaka kumsajili kwa ajili ya mazungumzo zaidi na sio kuomba avunje mkataba yeye mwenyewe kwa kulipa sehemu ya gharama

Kuna taarifa kuwa Inonga tayari alishafanya mazungumzo na Klabu ya FAR Rabat ya Morocco na imeelezwa akili yake iko huko

Hata hivyo Simba imetahadharishwa kuwa makini kwani hiyo FAR Rabat inaweza kuwa ya hapa hapa bongo

Msimu huu Inonga ameonyesha sura mbili tofauti wakati akiitumikia timu ya Taifa ya DR Congo na Simba

Inonga wa Simba hakuwa bora kama yule Inonga aliyeisaidia DR Congo kucheza nusu fainali ya michuano ya AFCON 2023 iliyofanyika Ivory Coast mwezi February

Wakati Simba ikipoteza mchezo dhidi ya Yanga SC kwa kufungwa mabao 5-1 Inonga alikuwa miongoni mwa wachezaji watano ambao walisimamishwa kwa tuhuma za kucheza chini ya kiwango

Hata Simba ilipopoteza mchezo wa pili kwa kufungwa mabao 2-1 Inonga tena akaingia katika tuhuma baada ya kucheza kwa takribani dakika 15 tu akidai kuumia

Inonga aliomba kutoka baada ya kuanguka wakati akiwania mpira katika tukio ambalo wengi wanadhani halikiwa la kumfanya aumie kiasi cha kuomba kutoka

Tangu mechi ya Yanga Inonga hakutumika tena licha ya kuwa fiti na kwa kuwa Simba haikuwa na mpango wa kumtumia katika mechi zilizobaki, wamemruhusu akashughulikie masuala yake lakini akirejea ahakikishe ameileta timu inayotaka kumsajili.

SOMA NA HII  LAKRED HATIANI KUIKOSA DABI YA KARIAKOO...SIMBA NA YANGA