Home Simba SC SIMBA KUTEKETEZA ZAIDI YA MILIONI 200 HUKO MOROCCO, MCHANGANUO UKO HIVI…

SIMBA KUTEKETEZA ZAIDI YA MILIONI 200 HUKO MOROCCO, MCHANGANUO UKO HIVI…


MSAFARA wa watu 20 wa Simba upo Morocco katika Mji wa Rabat kwenye moja ya hoteli ya kifahari kwenye eneo hilo.

Simba imejichimbia katika hoteli ya Dawliz Resort & Spa, ambayo kwa siku moja chumba cha watu wawili unatakiwa kulipa si chini ya Sh390,000.

Katika msafara huo kuna vyumba vitano ambavyo vitatumiwa na watu wa benchi la ufundi kila mmoja kulala cha kwake ambacho thamani yake si chini ya Sh400,000.

Kwa maana hiyo Simba kwa siku moja vyumba 15, ambavyo watalala watu wawili watakuwa wanalipia  TSh 5,850,000 kwa ajili ya kulala pamoja na kupata kifungua kinywa, hivyo kwa siku zote 15 watalipa Tsh 87,750,000

Vyumba vitano ambavyo watatumia benchi la ufundi kwa siku 15, watakazokuwa hapo Rabat watakuwa wanalipa si chini ya Tsh 30,000,000 .

Kwahiyo idadi ya watu zaidi ya ishirini waliokuwepo katika msafara huo ndani ya siku 15 watakazokuwa nchini humo kulala na kunywa chai watalipia si chini ya TSh 117,750,000  milioni.

Simba watalazimika kuingia gharama nyingine kama kunununua chakula na vinywaji kwa ajili ya mchana na usiku ndio maana wamesafiri na mpishi wao, Samuel Cyprian ambaye anawajulia vilivyo.

Wakati huo huo msafara huo utaingia gharama nyingine ya kulipia usafiri wa ndani, uwanja wa mazoezi na mambo mengine ya msingi.

Pesa hiyo inaweza kuzidi kwani juzi Agosti 12, msafara wa Simba awamu ya pili wa wachezaji pamoja na viongozi uliondoka Tanzania kuelekea Rabat kuungana na wenzao.

Ukilipa pesa hiyo unapata chai asubuhi bure ila chakula cha mchana na usiku msafara huo wa Simba unatakiwa kujitegemea wenyewe kitu ambacho kinaweza kuifanya bajeti ya kambi hiyo kuzidi Tsh 200,000,000 

SOMA NA HII  TAKWIMU ZAONGEA.....YANGA WANANAFASI YA KUBEBA UBINGWA AFRIKA KULIKO SIMBA...