Home Habari za michezo TAKWIMU ZAONGEA…..YANGA WANANAFASI YA KUBEBA UBINGWA AFRIKA KULIKO SIMBA…

TAKWIMU ZAONGEA…..YANGA WANANAFASI YA KUBEBA UBINGWA AFRIKA KULIKO SIMBA…

Habari za Michezo leo

Klabu ya Yanga imeipiku Simba kwenye orodha ya Klabu inayopewa nafasi ya kutwaa taji la Klabu bingwa Afrika.

Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na chombo maalum cha tafiti za soka (ASRI) Barani Afrika, Yanga imepewa asilimia 10 ikiwa katika nafasi ya 5 wakati Simba imepewa asilimia 6 ikiwa katika nafasi ya 7 kati ya Klabu nane zilizosalia.

Wakati Yanga wakipewa nafasi kuliko Simba,lakini wao ndio wenye mzigo mkubwa kwani wanakutana na Mamelodi Sundown ambayo ndiyo waliopewa nafasi ya kwanza kutwaa Ubingwa wakiwa na asilimia 24.

Simba ambayo imepewa nafasi finyu kuliko Yanga wamekabidhiwa Ahly waliopewa asilimia 20 kutwaa Ubingwa.

Mamelodi Sundonwns %24 VS Yanga SC %10
National Al Ahly %20 VS Simba SC %6
Esperance de Tunis % 14
Petro Atletico %12
ASEC Mimosas %6
TP Mazembe %6

SOMA NA HII  ISHU YA SIMBA KUACHANA NA ROBERTINHO, UONGOZI WAFUNGUKA HAYA