Home Habari za michezo PAMOJA NA KUISAIDIA YANGA SC CAF….WACHAMBUZI BONGO WAENDELEA KUMLALIA DJUMA….

PAMOJA NA KUISAIDIA YANGA SC CAF….WACHAMBUZI BONGO WAENDELEA KUMLALIA DJUMA….

Habari za Yanga SC

Kupitia #SportsArena ya #WasafiFm mchambuzi George Job amesema kuwa katika msimu huu wa 2022/23 kiwango cha beki wa kulia wa Yanga SC, Djuma Shaban kimeshuka tofauti na msimu uliopita.

“Ukiachana na Injury, performance ya Djuma imekuwa too flat msimu huu, hajawa yule wa msimu uliopita, msimu uliopita ulikuwa ukizungumzia right back ulikuwa unamtaja Djuma Shaban over hata Kapombe.

“Lakini kwa msimu huu unaweka question mark nyingi sana, kwenye mechi nyingi performance yake imekuwa flat sana nadhani anahitaji kuongeza juhudi.

“Kuna wakati alikuwa anazungumziwa uzito akapungua lakini bado hajarudi kwenye kiwango au ubora wake ambao watu wengi walikuwa wanauzungumzia,” amesema George Job.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA MAMELOD....YANGA WATOA KALI YA MWAKA....DICK JOB ATEMA CHECHE...