Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA MAMELOD….YANGA WATOA KALI YA MWAKA….DICK JOB ATEMA CHECHE…

KUELEKEA MECHI NA MAMELOD….YANGA WATOA KALI YA MWAKA….DICK JOB ATEMA CHECHE…

Habari za Michezo leo

Meneja wa Habari na mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Shabani Kamwe anasema kuwa anazo taarifa kutoka Afrika Kusini jinsi wanavyowazungumza Yanga SC.

Kamwe amesema hayo jana wakati akizindua hamasa kuelekea mchezo wa robo fainali ya CAFCL dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini utakaopigwa Jumamosi, Machi 30, 2024 katika Dimba la Mkapa majira ya saa 3:00 usiku.

“Juzi niligundua kuwa wengi wanaonunua tiketi za VIP wengi wanatoka nje ya nchi, kwa sababu tumepokea emails na simu nyingi kutoka Kenya, Uganda, Malawi na Zambia wakihitaji tiketi.

“Tumepata picha kwamba ukubwa wa hii mechi sio tu hapa Tanzania, hata mashabiki wa nchi za jirani wanataka kuishuhudia mechi yetu.

“Mechi yetu dhidi ya Mamelodi inazungumziwa Afrika nzima kwa sababu kwa sasa Mamelodi ndiyo timu yenye mvuto zaidi Afrika alafu Yanga ndiyo Suprise Package.

“Hata kwenye mijadala ya watu Afrika Kusini wanasema haupaswi kuichukulia poa Yanga kutokana na kile ilichokifanya msimu uliopita kwenye Kombe la Shirikisho kwa sababu wanaweza kukifanya kwenye Klabu Bingwa Afrika,” amesema Kamwe.

JOB ATIA NENO.

Beki wa Yanga, Dickson Job amesema wanaifahamu vizuri Mamelodi Sundowns na wapo tayari kwa ajili ya kuvaana nao Jumamosi hii. Job ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo amesema wanafahamu ubora wa Mamelodi, lakini kwao wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanakabiliana nao ndani ya uwanja.

“Mazoezi tunayofanya yatakwenda kutoa picha halisi tutawezaje kushinda na kuwazuia wapinzani wetu, kwa kutumia ubora wetu na kikosi kipana tulichonacho, tumevuka hatua ngumu nyingi na kushinda sehemu ambayo wengi hawakutupa nafasi.

“Jambo zuri tuna kocha anayeijua Mamelodi na ni lazima atatupa mbinu ya kuwamaliza kwani anawafahamu vizuri, kwa kweli hatutacheza kwa hofu ya kuangalia jina la mchezaji au nchi kwani tunachotafuta ni ushindi utakaotupa wepesi wa kutinga nusu fainali, tunaamini tuna uwezo mkubwa wa kushinda mechi hii,” alisema Job.

Comments:

SOMA NA HII  MASHINE HII HAPA.....YANGA WAITIBULIA AS VITA DILI LA KUMPATA....WAMTUMIA MKATABA 'CHAP' HARAKA...