Home Habari za michezo MASHINE HII HAPA…..YANGA WAITIBULIA AS VITA DILI LA KUMPATA….WAMTUMIA MKATABA ‘CHAP’ HARAKA…

MASHINE HII HAPA…..YANGA WAITIBULIA AS VITA DILI LA KUMPATA….WAMTUMIA MKATABA ‘CHAP’ HARAKA…

Tetesi za usajili yanga

YANGA imeitibulia AS Vita ya DR Congo baada ya kuizidi kete kwa kumnyakua winga kutoka Union Maniema, Basiala Agee, jambo lililomfanya kocha wa kikosi hicho Raoul Shungu aseme ameumizwa kukosa chaguo moja bora alilokuwa akilihitaji.

Japo hadi sasa Yanga haijatangaza rasmi kuhusu winga huyo Mkongomani, lakini habari za ndani zinasema mchezaji huyo alishatumiwa na mkataba na amemalizana na mabosi wake na wakati wowote ataibuka nchini, licha ya awali kuwa miongoni mwa mastaa muhimu wa kikosi cha Maniema.

Agee aliyefunga mabao matano na kuasisti tano msimu huu akiwa na kikosi hicho, inaelezwa alikuwa kwenye rada ya AS Vita, lakini akaamua kuwapotezea ili atue Yanga na Shungu aliyewahi kuwanoa mabingwa hao wa Tanzania, amekiri ameumizwa kwa kukosekana kwake.

Inaelezwa kama Yanga imemalizana na winga huyo itakuwa imeokota dodo kwenye mwarobaini kwani kutokana na sheria za CAF mchezaji huyo atacheza michuano ya kimataifa ambayo Yanga itaendelea nayo Februari mwaka huu.

Shungu alisema, sasa kikosi cha Yanga kimepata kiongozi mpya huku akisisitiza alitaka kumsajili winga huyo jambo ambalo lingekuwa faida kwa timu yake kwani kutokana na rekodi alizonazo angekuwa msaada mkubwa sana.

Alisema kuwa ukiachana na uongozi, hata yeye alikuwa na shauku ya kumpata na winga huyo kwani angemfaa kwa mambo mengi kubwa ni kujenga timu yenye uwezo wa kushinda muda wote, lakini wamezidiwa na Yanga aliyoihakikishia kwamba imelamba dume kwelikweli.

“Tumekosa mchezaji muhimu japo hajaenda timu mbaya, ni mchezaji ambaye hawezi kukosa mafanikio katika kikosi chochote, ni matamanio ya kocha yeyote kuwa na winga wa namna yake mwenye sifa kama za mshambuliaji anayeweza kukupa vitu vingi vya faida anapokuwa uwanjani,” alisema Shungu aliyeongeza;

“Uongozi ulikuwa tayari kabisa kumchukua lakini bahati haijawa kwetu, kama Yanga watamalizana naye basi tutaangalia anayefaa zaidi ili kwenda kuziba mapengo tuliyonayo japo hatutakataa ukweli kuwa chaguo la kwanza tumelikosa.”

Mapema wiki hii  mabosi wa klabu ya Yanga walituma mkataba winga huyo baada ya kumalizana na tajiri wa Maneama, Amissi Kumba ikiwa ni pendekezo la kocha Miguel Gamondi anayepambana kuivusha Yanga kwa mara ya kwanza kuingia robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu ilipobadilishwa mfumo mwaka 1997.

SOMA NA HII  MANARA: YANGA TUMEPOKEA OFA YA AL AHLY KUMTAKA NABI...KOCHA WA SIMBA KATUAIBISHA SANA...