Home Habari za michezo MANARA: YANGA TUMEPOKEA OFA YA AL AHLY KUMTAKA NABI…KOCHA WA SIMBA KATUAIBISHA...

MANARA: YANGA TUMEPOKEA OFA YA AL AHLY KUMTAKA NABI…KOCHA WA SIMBA KATUAIBISHA SANA…

Habari za Yanga

Msemaji wa Yanga Haji Manara amemzodoa kimtindo kocha wa Simba baada ya kwenda kwa mashabiki kushangilia sare wakati timu yake iko nyuma kwa kila kitu.

Kocha huyo anaejulikana kama Robertinho Olivieira alishangilia kwa nguvu bao ambalo Azam Fc walijifunga katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa juzi.

“Zamani nilivyokuwa mdogo nilijua kila Mdhungu ana maarifa kama Professor, nowadays najionea mazangaiza tu.

“Unawezaje kwenda kwa mashabiki kushangilia sare tena upo home na bado team yako imezidiwa points kibao na wanaoongoza ligi? Hili ndio tukio la aibu zaidi katika football wiki hii suniani, limeizidi hata lile la kurudi reverse.

“Na siku professor Nabi ambaye ni kweli juzi tulipokea offa ya kutakiwa na Al Ahly, akifanya kituko kama hiki asubuhi yake hafiki”

“Hili jambo la jana aibu tumeona sisi huku kitaani,” ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii,” amesema Manara.

SOMA NA HII  SHAFII DAUDA ATUPA JIWE LA GIZANI KWA MASTAA HAWA WA SIMBA....