Home Azam FC JINA LA KINDA WA AZAM FC, TEPSI EVANCE LATAJWA TENA …KOCHA ULAYA...

JINA LA KINDA WA AZAM FC, TEPSI EVANCE LATAJWA TENA …KOCHA ULAYA APAGAWA BAADA YA KUONA VIDEO…


KIWANGO cha winga wa Azam FC, Tepsi Evance kimemkosha kocha wa Ligi daraja la Tatu huko Ufaransa ‘Championnat National’, Emmanuel Da Costa.

Da Costa ambaye ni kocha wa US Creteil-Lusitanos, alisema anavutiwa na uchezaji wa winga huyo kiasi cha kumfananisha na Jeremy Doku wa Stade Rennais.

“Kuna mambo ambayo nadhani wanafanana na Doku, kama hamfahamu huyo mchezaji basi ni vizuri kutenga muda wako na kumfuatilia, kuna mambo ambayo anapaswa kuongeza ili kuwa bora zaidi tena zaidi ya hata huyo ambaye namfananisha naye,” alisema.

Kwenye michezo sita ambayo ameichezea Azam FC, Tepsi mwenye miaka 19 amepachika bao moja ambalo lilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting na kutoa asisti mbili, ikiwemo moja ambayo ilikuwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa Mzambia, Rodgers Kola.

Da Costa aliipata video ya Tepsi baada ya kutumiwa na miongoni mwa wadau wa Nje ya Bongo (jina tunalo) aliyekaribu na kocha huyo kwa lengo la kuona vile ambavyo Tanzania imebarikiwa wachezaji wengi tena wenye vipaji vya hali ya juu.

Licha ya kumsifu winga huyo, alimtaka kukaza uzi na kupigania nafasi ya kwenda Ulaya maana kiwango cha soka la huko kinaweza kumfanya kuwa bora zaidi.

“Ana nafasi ya kuendelea kukua, ukubwa wa ligi unaweza kusaidia mchezaji kukua kiwango, anapaswa kuwa na mtazamo wa mbali,” alisema kocha huyo.

Azam imeanza kumtumia Tepsi baada ya kuumia kwa baadhi ya nyota wao wa eneo la ushambuliaji.

SOMA NA HII  IBENGE APANIA KUMNYOFOA INONGA MSIMBAZI...MABOSI SIMBA WAKUBALI KUMWACHIA...