RAM siku hizi imekuwa feature ya muhimu kutokana na program nyingi kwenye simu za kisasa kuhitaji nguvu kubwa ya uendeshaji. Simu mpya za kama aina ya Infinix NOTE 11 Pro yenye 8GB RAM itaweza kuwa na uwezo wa kuruhusu kuongezeka RAM hadi 5GB kwa kugusa kitufe tu inatoka 8GB RAM na kuwa 13GB RAM (8GB RAM+5GB RAM = 13GB RAM).
Haya ni mapinduzi ya kitekinolojia ambapo sasa utaweza kutumia Applications nyingi kwa wakati mmoja bila kumaliza chaji ya simu haraka wala kustaki, Kuongezeka kwa RAM kutakusaidia kuweza kufungua Apps nyingine kwa wakati mmoja kwa kasi kutoka 802ms mpaka 307ms ambapo kasi imeongezeka kwa asilimia 61%.
Utendaji wa RAM wa NOTE 11Series unapatikana kwenye Infinix NOTE11 Pro / NOTE 11. Kwa kuwasha RAM Iliyoongezwa, simu inaweza kupakia games kwa kasi na kuhakikisha kuwa watumiaji wanaweza kuanza mchezo mara moja, hata ikiwa utabadili na kufungua programu nyingi.
Hizi hapa hatua nne za kufuata kuongeza RAM kwenye simu za NOTE 11Series.
1️⃣Click Setting
2️⃣Find Special Function
3️⃣Tap MemFusion
4️⃣Turn on MemFusion and choose how much RAM you want to add
5️⃣Restarting to make it run
Infinix Imekuwa ikija na kuanzisha teknolojia kubwa na mpya kwenye simu zake na bado simu zake zimekuwa zikiuzwa kwa bei rafiki, RAM kuogezeka ni moja ya teknolojia ambayo Infinix wamepanga kuifanya endelevu kwa simu zote zijazo. Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa za Infinix Tanzania @infinixmobiletz kupata ufafanuzi zaidi.