Home Habari za michezo SHOMARI KIBWANA AFUNGUKA ISHU YA KUSEPA YANGA

SHOMARI KIBWANA AFUNGUKA ISHU YA KUSEPA YANGA

SAFARI YA KIBWANA JANGWANI KIZUNGUMKUTI...LOMALISA AUNGUZA KIBANDA...SIJUI ITAKUAJE?

Menejimenti ya mlinzi Shomari Kibwana kupitia kwa meneja wake George Job amesema hawana mpango wa kuondoka Yanga SC licha kuwa mchezaji amekosa nafasi ya kucheza bali wanachoangalia ni kubaki Yanga SC na kuipambania timu hiyo kubeba mataji waliyobeba msimu uliopita.

Yanga ilimsajili wa beki Kibwana Ally Shomari kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, mnamo Agosti 9, 2020 na alionyesha kiwango kizuri lakini ujio wa beki raia wa Ivory Coast, Kouassi Attohoula Yao umefifisha matumaini ya kijana wa Morogoro kuendelea kuwa tegemeo kwenye kikosi cha Yanga.

“Kwanza hatuna taarifa hiyo kutoka kwa klabu kama tunapaswa kuondoka kwa mkopo na sisi pia hatuna huo mpango wa kutoka kwa mkopo, Tupo mpaka mwisho wa msimu huu kuisaidia timu kutetea mafanikio ya msimu jana,” amesema Meneja wa Shomari Kibwama, George Job.

SOMA NA HII  GAMONDI AWEKA MPANGO YAKE MEZANI DHIDI YA SINGIDA