Home Habari za michezo KAMA ULIKUWA HUJUI HIVI NDIO VIGOGO WALIVYOWEKEZA YANGA

KAMA ULIKUWA HUJUI HIVI NDIO VIGOGO WALIVYOWEKEZA YANGA

YANGA imebakiza siku tano kabla ya kushuka uwanjani kuanza kazi kwenye mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kuna mambo mazito mabosi wao wamewaandalia.

Yanga itafungua pazia la mechi hizo watakapokutana na CR Belouzdad ya Algeria mechi ambayo itapigwa Novemba 24 nchini humo na mabingwa hao wa Tanzania wakati wowote kuanzia Novemba 21 wataondoka nchini kuwafuata Waarabu hao.

Kabla ya kutimka kwa kikosi hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Rodgers Gumbo ameliambia Mwanaspoti kuwa wao kazi yao wameshamaliza na msimu huu kutakuwa na maboresho ya posho zao za mechi kwa viwango .

Gumbo ambaye ameiongoza kamati hiyo kuchukua mataji sita pamoja na Yanga kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika alisema uongozi wa klabu chini ya mfadhili wao Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ watakuwa na mgawanyo uleule wa posho kwa ushindi wa ugenini, sarte ya ugenini, pia kushinda nyumbani.

Kigogo huyo alisema mabadiliko ya msimu huu utakuwa kwenye viwango na wamekubaliana kuviboresha kutokana na ugumu wa ligi ya mabingwa wakitaka wachezaji wao kuwa na umakini zaidi.

“Tunahitaji kushinda mechi zetu za ugenini na nyumbani, pia kama utashindwa kushinda ugenini angalau upate sare kuliko kupoteza kwahiyo sarte ya ugenini nayo itakuwa na kitu lakini sare ya nyumbani au kupotezxa hiyo hakuna kitu,” alisema Gumbo.

“Uongozi unataka kuona Yanga inabaki kwenye ubora wake wa matokeo kama ambavyo tulifanya msimu uliopita kwenye shirikisho, kama wachezaji wetu shida yao fedha basi kazi ni kwao, hivi viwango tutawatangazia wao kwanza kabla yoyote.

Aidha Gumbo aliongeza kuwa uongozi wao umefanya uwekezaji mkubwa kwenye kikosi chao hatua ambayo sasa inawarahisishia kupata matokeo kuliko kuwekeza nje ya uwanja.

“Klabu imefanya uwekezaji mkubwa kwenye kikosi chetu kuliko eneo lolote, zipo timu wao wanawekeza nje ya uwanja, sisi tumesajili vizuri, tumeunda benchi zuri la ufundi lakini mkifika kambini kwetu mazoezini mtaona jinsi mambo yanavyoendeshwa kisasa, mazingira haya yote hayatushtui kuona tunapata matokeo haya.”

SOMA NA HII  MORISSON AGONGELEA MSUMALI WA MOTO YANGA...AZIZ KI AWAJIBU KIROHO MBAYA