Home Habari za michezo KUELEKEA KARIAKOO DABI KESHO….’BEKI LA KAZI’ YANGA AWAIBIA SIRI MASTAA WA SIMBA…

KUELEKEA KARIAKOO DABI KESHO….’BEKI LA KAZI’ YANGA AWAIBIA SIRI MASTAA WA SIMBA…

Habari za Michezo

Beki wa zamani wa Yanga, Ladslaus Mbogo ameangalia kasi na ubora wa Maxi Nzengeli, Azizi KI na Pacome Zouzoua waliokuwa nao kwa sasa ambapo amekiri wazi kuwa mabeki na viungo wakabaji wa Simba wanatakiwa kuwa makini sana katika mchezo wao wa jumapili kwani wakifanya masihara watapigwa mabao nyingi.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ambao unawakutanisha wababe hao wa soka la Tanzania utapigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam saa 11 jioni ambapo Yanga na Simba wanalingana pointi 18 kila mmoja wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Mbogo amesema safu ya ulinzi ya Simba hivi karibuni imekuwa ikifanya makosa ambayo yamekuwa yakifanya wafungwe mabao ya kizembe katika mechi zake walizocheza kitu ambacho katika mchezo wao wa jumapili wanatakiwa kuwa makini sana lasivyo watafungwa.

Beki huyo aliyekipiga Yanga kwa msimu mmoja wa 2012/13, amesema Yanga ya sasa iko katika ubora mkubwa haswa wanapokuwa wakishambulia kitu ambacho anaona kitakuwa kigumu sana kwa Simba ambayo imekuwa ikifanya makosa yanayojirudia haswa kwa mabeki wake.

“Ukimwangalia Maxi, Azizi KI, Zouzoua na kikosi kwa ujumla cha Yanga kipo katika ubora mkubwa hivyo Simba wasipokuwa makini haswa kwa mabeki wake ambao wamekuwa wakiruhusu wafungwe mabao rahisi basi huu mchezo utakuwa mgumu sana kwao.

“Lakini kama wakiwa makini basi ngoma itakuwa ngumu kwa Yanga maana Simba wako vizuri ukiacha mapungufu madogo waliyokuwa nao walinzi wake ambayo yanarekebishika,” amesema Mbogo ambaye kwa sasa amestaafu kucheza soka la ushindani.

SOMA NA HII  PICHA LA KUTISHA LAANZA KWA MORRISON ...BAADA YA NABI KUMUONA TU...KAGUNA KISHA AKAMPASUKIA UKWELI WAKE...