Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO….ZAHERA ‘KAFUNGA MACHO’ KISHA AKATABIRI MSHINDI WAKE…

KUELEKEA MECHI YA KESHO….ZAHERA ‘KAFUNGA MACHO’ KISHA AKATABIRI MSHINDI WAKE…

Habari za Habari

Aliyekuwa kocha wa Coastal Union, Mwinyi Zahera anasema timu zote zinacheza soka la tofauti kulingana na mbinu za makocha wanavyotaka zicheze.

Zahera anasema Simba licha ya kucheza soka la taratibu, imekuwa inacheza mpira wa pasi na hutulia kupanga mashambulizi, na kwamba mbinu zao hizo hatashangaa kama zitaipa ushindi.

Akiizungumzia Yanga, Zahera anasema inacheza soka tofauti na Simba ikiwa inacheza la kasi ikikaba kwa nguvu na kufanya mashambulizi ya haraka.

“Timu zote zinacheza kwa utofauti mkubwa. Unawaona Simba wao wanacheza soka la taratibu. Wanacheza mpira wa pasi na wanashinda na inaonekana wanaitendea haki falsafa ya kocha wao,” anasema kocha huyo.

“Simba hawaonekani kupata shida, ndio maana unaona walicheza hivyo walipokutana na Al Ahly na walicheza mpira mkubwa kwa mbinu hizohizo na kama wakirudia kiwango kile Jumapili itakuwa mechi ngumu.

“Yanga wako tofauti na Simba wao wanakaba sana na wana kasi ya kumalizia mashambulizi yao. Ile kasi yao inawafanya wapinzani kushindwa kujipanga haraka. Wachezaji wa Yanga wana akili, ubora na mbio ndio maana unaona wanafika kwa idadi kubwa eneo la wapinzani na wanafunga.

“Hii mechi itakuwa ngumu sana na mimi naona itaamuliwa kwa makosa madogo ya kibinadamu kwa wachezaji. Ambaye atashindwa kumdhibiti mwenzake vizuri atajikuta anapoteza. Pia sioni kama itakuwa mechi ya mabao mengi sana.”

Goran Kopunovic (Tabora United)

Kocha wa Tabora United, Goran Kopunovic anasema ingawa hajapata muda wa kuzifuatilia kwa muda mrefu timu hizo mbili, kwake anaamini itakuwa mechi ngumu lakini itaamuliwa na ubora wa mbinu za makocha na ubora wa wachezaji.

“Nimekuwa natumia muda mwingi kuangalia wapinzani ninaokutana nao kwenye ligi, ni mara chache sana kuziona hizo klabu mbili, lakini haitakuwa mechi rahisi. Kwa timu yoyote nadhani kocha ambaye atafaulu kwa mbinu dhidi ya mwenzake atashinda au upande ambao wachezaji wake watacheza kwa ubora,” anasema Goran ambaye amewahi kuifundisha Simba akiifunga Yanga mara moja.

SOMA NA HII  PAMOJA NA 'KUWAZAGAMUA' WASUDAN JUZI...MASTAA YANGA WAPEWA ONYO KWA NAMUNGO...