WACHEZAJI 10 wa Klabu ya Simba leo wataibukia nchini Kenya kwa ajili ya kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen.
Stars imeweka kambi Kenya kwa ajili ya maandalizi ya kufuzu Afcon na Machi 15 ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya na ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Kesho ina kazi nyingine ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya ambapo wachezaji hao wa Simba pia wanatarajiwa kucheza mchezo huo.
Nyota hao wa Simba ambao jana Machi 16 walikuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Al Merrikh ya Sudan na kushinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa ni pamoja na :-Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein,’Zimbwe’ Kennedy Juma.
Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Said Ndemla na John Bocco.
Ni 7 kati ya 10 ambao wameitwa Taifa Stars jana walicheza mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Watatu hawakucheza ambao ni nahodha John Bocco, kiungo Said Ndemla na Hassan Dilunga.