Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHI NA SIMBA….MATAJIRI YANGA WAITANA ‘FASTA’ KUMALIZIA KAZI…

KUELEKEA MECHI YA KESHI NA SIMBA….MATAJIRI YANGA WAITANA ‘FASTA’ KUMALIZIA KAZI…

Habari za Yanga

Yanga wanaonekana kuutaka mchezo wa Kariakoo Dabi, ni baada ya Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, yenye watu nane imepanga wamekutana Jumatano kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi kuelekea mchezo huo.

Dabi hiyo inatarajiwa kuzikutanisha timu hizo kongwe za Simba dhidi ya Yanga ambayo itapigwa Jumapili hii saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo ya mashindano, inaongozwa na Matajiri wakubwa hapa nchini wakiongozwa na Mwenyekiti, Rogers Gumbo, Seif Magari, Mustapha Himba, Lucas Masahauri, David Mosha, Majid Suleiman, Pelegrinus Rutayuga pamoja na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said mwenyewe.

Taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, matajiri wamepanga kukutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya ushindi kabla ya kufanya kikao na wachezaji siku moja kabla ya mchezo huo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa katika kikao, kikubwa kitakachojadiliwa kuiandaa timu sambamba na kuwapa hamasa na morali itakayowafanya wacheze kwa kujituma ili wapate ushindi.

SOMA NA HII  RASMI...AZAM FC WANYOOSHA MIKONO JUU UBINGWA WA LIGI KUU...WAFUNGUKA SABABU YA NDOTO KUYEYUKA...