Home Habari za michezo KAPOMBE AFUNGUKA WALICHOFANYIWA MASTAA WA SIMBA KUELEKEA MECHI NA YANGA KESHO…

KAPOMBE AFUNGUKA WALICHOFANYIWA MASTAA WA SIMBA KUELEKEA MECHI NA YANGA KESHO…

Habari za Simba

Mlinzi wa kulia ambaye ni mchezaji mwandamizi ndani ya kikosi cha Simba, Shomari Kapombe amesema wamepata maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga.

Kapombe amesema wiki moja waliopata ya kujiandaa na mchezo huo mkubwa Afrika yametosha na anaamini watafanikiwa kupata ushindi.

Mlinzi huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi za Derby amesema inapofika siku kama ya kesho huwa hana presha na anajitahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu kupata ushindi.

Kapombe amesema wachezaji wanafahamu mchezo huo umebeba hisia za mashabiki hivyo watahakikisha wanapambana ili kuwapa furaha.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari, tumepata wiki moja ya maandalizi ambayo inatufanya tuwe tayari kwa mchezo wa kesho.

“Tunafahamu mchezo wa kesho una presha kubwa na unabeba hisia kwa mashabiki na huwa unatazamwa sana sisi wachezaji tumejiandaa kwa kila kitu kuhakikisha tunashinda na kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Kapombe.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AYAKUBALI MABAO YA AZAM FC,MABEKI WAKINGIWA KIFUA