Home Habari za michezo MBRAZILI SIMBA AZIIDI KUITEMEA NYONGO YANGA…AJIFANANISHA NA ‘WAKUBWA WENGINE’..

MBRAZILI SIMBA AZIIDI KUITEMEA NYONGO YANGA…AJIFANANISHA NA ‘WAKUBWA WENGINE’..

Habari za Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa ataingia kwenye mchezo wa kesho wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani wa jadi ya Yanga kwa lengo la kupambana kupata alama tatu.

Robertinho amesema timu kubwa siku zote lengo lake ni kuhakikisha inapata pointi tatu katika kila mchezo na hilo ndilo amejipanga kulifanya kesho.

Robertinho amesema anaiheshimu Yanga ni timu bora na siku zote Derby haitabiriki lakini anamatumaini makubwa na wachezaji wetu pamoja na maandalizi waliyopata.

Robertinho ameongeza kuwa amekuwa akiamini mpira wa miguu unatakiwa kucheza vizuri na kushinda na hiyo ndio falsafa yake.

“Mechi ya Derby siku zote haitabiriki. Derby inaamuliwa baada ya dakika 90 za mchezo, tunaiheshimu Yanga lakini tutaingia kwenye mchezo kwa lengo la kutafuta pointi tatu.

“Ninawaamini wachezaji wangu, wana vipaji vikubwa na tumejipanga kushinda. Sina presha ya mechi ya kesho, ni kama michezo mingine lakini kupata pointi tatu ndicho kipaumbele chetu,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  HAZIRA ZA SOPU ZAHAMIA KWA MANULA WA SIMBA...DENI LAKE LAZIDI KUKUA KILA SIKU....