Home Habari za michezo UCHAGUZI MKUU YANGA: DK MSOLA AWAPA ‘ZA USO’ WANACHAMA UKUMBINI…..ATAJA SABABU ZA...

UCHAGUZI MKUU YANGA: DK MSOLA AWAPA ‘ZA USO’ WANACHAMA UKUMBINI…..ATAJA SABABU ZA KUJIWEKA KANDO ….


MWENYEKITI anayemaliza muda wake Mshindo Msola amewataka wajumbe kufanya maamuzi sahihi katika uchaguzi wa viongozi wao watakaoiongoza vyema timu yao.

Msola ameyasema hayo leo wakati akitoa neno kwa Wanayanga katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere unapofanyika uchaguzi.

Msola amesema anaamini kura zikienda kwa watu sahihi itasaidia kuendeleza pale ambapo yeye na wajumbe wanaomaliza muda wao walipiishia.

“Sitegemei kugombea nafasi yoyote, nitabakia kuwa mwanayanga mwaminifu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu,” anasema Msola.

Aidha Msola amewatakia kila la heri waliokuwa wajumbe wenzake ambao wamejitosa kuwania nafasi hizo kwa mara nyingine akiamini wanaweza kutokana na kazi kubwa walioifanya.

“Leo ni siku muhimu sana katika maisha yangu maana katika kampeni zangu nilitaka suala la mabadiliko ya kiuendeshaji na leo ndio uchaguzi unaenda kuwaweka viongozi hao madarakani ni jambo la kujivunia sana sana”. amesema Msola.

SOMA NA HII  FT: YANGA 1-0 KMC FC ....FEI TOTO AMUOKOA NABI DK ZA MCHANA...MAYELE AKOSA REKODI MPYA...