Home Uncategorized AS KIGALI LAZIMA WAKE LEO

AS KIGALI LAZIMA WAKE LEO


JACKSON Mayanja, Kocha Mkuu wa KMC amesema kwa sasa kikosi kipo sawa kumalizana na AS Kigali ya Rwanda kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

KMC itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya AS Kigali baada ya mchezo wa kwanza kutoka suluhu nchini Rwanda huku waamuzi wa mchezo huo wakiwa wanatoka Sudan, ina kazi ya kusaka ushindi ili kusonga mbele.

Mayanja alisema: “Tumecheza nao mchezo wa kwanza nimetambua mbinu zao, wanakuja nyumbani hawatanisumbua ni lazima tutumie nafasi hiyo kushinda tena mapema.

“Licha ya kukosekana kwa washambuliaji halisi kama Salim Aiyee na Ramadhani Kapera, hainipi tabu, nina kikosi kipana nitawabadili wengine wavae jukumu hilo,” alisema Mayanja

SOMA NA HII  TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YAPIGA MTU MKONO AFRIKA KUSINI