Home Habari za michezo BAADA YA KUONA MAMBO YANAZIDI KUWA MAGUMU…KOCHA SIMBA AKUBALI YAISHE..AWAPA UBINGWA YANGA…

BAADA YA KUONA MAMBO YANAZIDI KUWA MAGUMU…KOCHA SIMBA AKUBALI YAISHE..AWAPA UBINGWA YANGA…


KOCHA Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana, mwenye historia na Simba, amekubali na kukiri kuwa msimu huu ubingwa wa Ligi Kuu Bara utakwenda Jangwani.

Hitimana alikuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, mwaka jana na baadaye akaja kuwa msaidizi wa Didier Gomes, kabla hajatimkia KMC Januari, mwaka huu.

Simba imetawala ubingwa wa ligi ikiutwaa kwa misimu minne mfululizo, lakini safari hii wameshaachwa kwa tofauti ya pointi 11 dhidi ya Yanga ingawa Simba wana kiporo kimoja.

Juzi Yanga iliwachapa KMC 2-0 kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara wikiendi iliyopita Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatatu baada ya mchezo huo, Hitimana alisema: “Yanga ni timu ambayo inapata matokeo mazuri kwa kila mechi inayocheza kwa msimu huu, sisi tulikuwa na madhaifu kwa upande wa mabeki wetu, licha ya sisi kupata nafasi nyingi za kufunga ila tukakosa, inabidi kujipanga kwa ajili ya mchezo ujao.

“Kwa asilimia 80% Yanga wana uwezo wa kuchukua ubingwa msimu huu kutokana na uwezo wao ndani na nje ya uwanja.”

Hitimana aliongeza kuwa msimamo wa ligi unatoa picha bingwa wa msimu huu nani.

“Lipo wazi kabisa hilo la ubingwa, kwa kifupi ni kuwa bingwa tayari ameshajulikana hadi hivi sasa, msimamo wa ligi unaonyesha.

“(Yanga) tangu kuanza kwa ligi imeonekana kucheza katika kiwango bora, imekuwa ikipata matokeo mazuri ya ushindi hata kama ikicheza kiwango kibovu.

“Kwetu sisi KMC tunapambania kumaliza ligi katika nafasi za katikati katika msimamo, lakini siyo ubingwa kwani tulikuwa na tatizo kubwa kwenye eneo la ulinzi na ndio maana tumepata shida kubwa, hatukuwa bora kwenye ulinzi na Yanga wametuadhibu kwa hilo,” aliongeza Hitimana.

SOMA NA HII  MWAKALEBELA 'AMPIGA NA KITU KIZITO' NABI..."..HATA LIGI TUTATAPOTEZA KWA SIMBA..."