Home Habari za michezo MWAKALEBELA ‘AMPIGA NA KITU KIZITO’ NABI…”..HATA LIGI TUTATAPOTEZA KWA SIMBA…”

MWAKALEBELA ‘AMPIGA NA KITU KIZITO’ NABI…”..HATA LIGI TUTATAPOTEZA KWA SIMBA…”

Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amesema timu hiyo ina kibarua kigumu cha kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini amemtaka Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi nguvu na akili nyingine aziongeze katika Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo aliitoa kabla ya juzi Jumatano Yanga kucheza mchezo wa kwanza wa Play-Off katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia uliochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga imeangukia kwenye michuano hiyo baada ya kuondolewa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Mwakalebela alisema anafahamu jukumu zito walilonalo kimataifa, lakini hiyo haifanyi kusahau michezo ya ligi.

Mwakalebela alisema kama nguvu kubwa ikielekezwa kimataifa, basi upo uwezekano wa kupoteza taji lao la ubingwa wa ligi ambalo wanalitetea msimu huu.

Aliongeza kuwa, Kocha Nabi anatakiwa kufanya maandalizi ya ligi na kimataifa ndani ya wakati mmoja kwa lengo la kutotoka kileleni ambako wamewaondoa watani wao, Simba SC.

“Presha ipo kubwa katika timu hivi sasa, hiyo ni baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kuangukia Shirikisho, hivyo kocha, wachezaji na viongozi wanatakiwa kujiongeza.

“Ninafahamu kwamba hivi sasa Yanga wanataka kuthibitisha ubora wao kwa kufuzu makundi Shirikisho wakitumia nguvu na akili nyingi.

“Hivyo hawatakiwi kufanya hivyo wakajisahau, badala yake kuipa umuhimu michezo ya ligi pia kwa lengo la kutetea ubingwa wetu, kwani Simba wanasubiri tuteleze kidogo ili watupoke ubingwa msimu huu,” alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  WAKATI HOROYA WAKIPANIA KUMALIZA KAZI DAR...MBRAZILI SIMBA KUINGIA NA SAPRAIZI HII ...