Home Uncategorized MEDDIE KAGERE AMJIBU KIBABE BOSSI WAKE SVEN

MEDDIE KAGERE AMJIBU KIBABE BOSSI WAKE SVEN


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba ameamua kumjibu kibabe bosi wake mkubwa kwenye benchi la ufundi Sven Vandenbroeck wakati huu wa maambukizi ya Virusi vya Corona akiwa nchini Rwanda.
Video ya Sven iliyotupiwa kwenye Ukurasa wa Instagram wa Simba ilimuonyesha akipiga danadanda ambapo alipiga jumla ya danadanda 32 mshambuliaji wake namba moja aliamua kumlipa kwa kutuma video ambayo alipiga danadanda 52.
Kwa sasa wachezaji wengi pamoja na makocha wamekuwa wakishinda nyumbani kuendelea na mazoezi binfasi ili kujiepusha na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimezidi kuwa janga la dunia.
Wakati ligi ikisimamishwa Sven alikiongoza kikosi hicho kwenye jumla ya mechi 18 za ligi ambapo alishinda mechi 15,sare moja na kufungwa mechi mbili.
SOMA NA HII  VIDEO: MIAKA 56 YA MAPINDUZI CHEKI KOMANDO ALIVYOMWAGIWA PILIPILI