Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA AL HILAL…HAWA HAPA MASTAA TISA WATAKAOKOSEKANA….MATOLA...

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA AL HILAL…HAWA HAPA MASTAA TISA WATAKAOKOSEKANA….MATOLA AVUNJA UKIMYA…


Kocha Msaidizi wa Kikosi cha Simba SC, Selemani Matola amesema wapo tayari kwa mchezo wa pili na wa mwisho wa Michuano Maalum huko nchini Sudan, utakaowakutanisha na wenyeji wao Al Hilal.

Simba SC iliyodhamiria kurejesha heshima ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara na kufika mbali kwenye michuano ya Kimataifa, itacheza mchezo huo kwenye mji wa Omdurman, huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 4-2 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.

Matola amesema wamejiandaa vizuri kuwakabili Al Hilal na wanaamini mchezo huo utaendelea kuwasaidia wachezaji wao kujiimarisha kuelekea michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayofuata na Michuano ya Kimataifa ambayo itaanza kurindima mwishoni mwa juma lijalo.

Kocha huyo mzawa amesema Benchi la Ufundi linaendelea kufurahia fursa waliyopata ya kushiriki Michuano ambayo inawapa nafasi baadhi ya wachezaji waliokosa maandalizi ya pamoja ya Pre Season ambapo waliweka Kambi Misri na wengine waliokosa nafasi ya kucheza michezo miwili ya awali ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold FC na Kagera Sugar.

“Kocha (Zoran Maki) sasa ameanza kupata picha halisi ya mchezaji fulani yuko vipi na amtumie wapi, hii itatusaidia sana kwenye michezo ya Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu wachezaji wanazidi kuimarika,” amesema Matola.

Simba SC inacheza michuano hiyo bila ya nyota wake tisa walioko katika kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars), pamoja na Erasto Nyoni ambaye ni mgonjwa na Joash Onyango aliyeachwa hapa nchini.

Katika mchezo wa kwanza kwenye michuano hiyo, wenyeji Al Hilal, walipata ushindi mnono dhidi ya Asante Kotoko mabao 5-0.

Habari njema ni kwamba kiungo mkabaji, Sadio Kanoute, amejiunga na kikosi hicho akitokea kwao Mali alipokwenda kufuatilia suala ya hati za kusafiria.

Endapo Simba SC itashinda mchezo wa leo, basi itakuwa bingwa wa michuano hiyo maalum, lakini ikitoka sare au kufungwa itakuwa imeshika nafasi ya pili nyuma ya wenyeji, Al Hilal.

Januari mwaka jana (2021) Simba SC iliwaalika Al Hilal na TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kushiriki michuano maalum iliyojulikana kwa jina la Simba Super Cup na wenyeji walitwaa ubingwa.

SOMA NA HII  DK MSOLA: SINA BUDI KUKAA KANDO YANGA....AFUNGUKA KWA HISIA SAKATA LA UCHAGUZI NA NAMNA MAMBO YALIVYO...