Home Uncategorized SIMBA YASHINDA MABAO 3-1 MBELE YA CHIPUKIZI

SIMBA YASHINDA MABAO 3-1 MBELE YA CHIPUKIZI

 


KIKOSI cha Simba kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola kimeanza kwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi.

Simba imeshinda mabao 3-1 mbele ya Chipukizi ambayo imefungasha virago jumla kwenye mashindano hayo kwa kuwa imepoteza mechi mbili mfululizo.


Mabao manne yaliyofungwa leo Uwanja wa Amaan yalifunguliwa na nyota wa Chipukizi Fakhi Mwalimu dakika 36 huku Simba ikiweka usawa kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 45.


Miraji Athuman ambaye amekuwa nyota wa mchezo wa leo kwa kusepa na laki mbili alipachika mabao mawili leo kipindi cha pili.


Alianza kupachika bao la pili kwa kichwa dakika ya 53 kwa pasi ya Kagere na lile la pili alipachika dakika ya 83 na kuifanya Simba kuanza kwa ushindi leo.

SOMA NA HII  BEKI WA LIVERPOOL KUTIMKIA ARSENAL