Home Habari za michezo CHICO USHINDI APATA MTETEZI MPYA YANGA….DAKTARI MTUNISIA AANIKA KILA KITU KINACHOMSIBU…

CHICO USHINDI APATA MTETEZI MPYA YANGA….DAKTARI MTUNISIA AANIKA KILA KITU KINACHOMSIBU…


Mashabiki wa Yanga bado hawamuelewi Chico Ushindi kutokana na rekodi yake ya kuwa majeruhi na ile ya kucheza, lakini mtaalam wa mazoezi ya viungo wa timu hiyo, Helmy Gueldich ameweka wazi kila kitu juu ya mshambuliaji huyo mpya.

Akizungumza, Helmy alisema kama kuna shabiki wa Yanga ana wasiwasi juu ya uwezo wa Ushindi anakosea vibaya na kwamba staa huyo mwenye kipaji kikubwa atawashangaza kila mmoja atakapomaliza programu yao.

Helmy alifafanua zaidi akisema kitu kinachomnyima Ushindi nafasi ya kusomeka ndani ya Yanga ni ishu ya kukosa maandalizi bora ya mwanzo wa msimu akiwa na Mazembe baada ya kukosa sehemu kubwa ya mechi za timu hiyo kutokana na nia yake ya kutaka kuondoka.

Kocha huyo aliongeza kuwa staa huyo ana tofauti kubwa ya ufiti wa mwili ukilinganisha na mastaa wenzake wa kikosi cha Yanga aliowakuta na wanachokifanya sasa ni kumpandisha ubora taratibu ili aweze kurejesha makali yaliyompaisha DR Congo.

“Najua watu hawamuelewi Ushindi, mimi nimecheza soka, nasema leo na mashabiki wa Yanga wachukue ninachokisema, Ushindi ni mmoja kati ya mastaa wakubwa tulionao sasa katika timu hii na ili waamini hilo ni suala la muda tu,” alisema Helmy ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga kutokana na mzuka alionao katika kuipenda kazi yake na pia anavyoshangilia mabao ya timu hiyo sambamba na wachezaji.

“Ushindi inawezekana alipata mwanzo mzuri wa maandalizi ya msimu akiwa na Mazembe (pre season) lakini alipoanza msimu kuna kipindi alionekana kukosa mechi na hii imetokana na kwamba alikuwa anataka kuondoka muda mrefu,” alisema Helmy.

Daktari wa viungo Youssef Mohamed aliongeza katika majeruhi ya sasa ya Ushindi tayari ameshakuwa sawa sambamba na kiungo Feisal Salum ambapo wawili wao wana uhakika hata kuwahi mechi ijayo ya ligi dhidi ya Namungo Aprili 23 Kwa Mkapa.

SOMA NA HII  MCHONGO CHAP HUU HAPA...KAMATA NJIA RAHISI YA KUSHINDA SLOT YA ROULETTE LEO...