Home Habari za michezo KISA MAFANIKIO YA SIMBA CAF….MTANGAZAJI AZAM TV ALAZIMIKA KUIOMBA MSAMAHA YANGA…

KISA MAFANIKIO YA SIMBA CAF….MTANGAZAJI AZAM TV ALAZIMIKA KUIOMBA MSAMAHA YANGA…


Mtangazaji wa Azam TV, Timzo Karugira amewaomba radhi viongozi, wachezaji, mashabiki wa Yanga na wapenzi wa mpira nchini kutokana na matamshi yake ya jana kuwa Yanga wameingia katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa mgongo wa Simba Sc, kauli ambayo imeibua mjadala mzito.

Akitangaza jana kabla ya mchezo wa Yanga na Zalan FC ya Sudan Kusini kuanza, Timzo alisema Yanga wameingia katika mashindano ya CAF baada ya kubebwa na watani zao Simba ambao walifanya vizuri katika mashindano hayo msimu uliopita na kusababisha Tanzania kupewa nafasi ya timu nne kushiriki mashindano ya Kimataifa ikiwemo Yanga.

Leo Jumapili, akifuta kauli hiyo, Timzo Karugira amesema Yanga wameingia CAF Champion League kama bingwa wa nchi msimu uliopita (2021/22) tena wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja na siyo kwa mgongo wa watani zao Simba kama alivyosema jana, hivyo alikosea na ameomba Yanga wamsamehe.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA KUSHUKA UWANJANI...PABLO AIBUKA NA JIPYA SIMBA..AFUNGUKA HALI ILIVYO...