Home Habari za michezo SIMBA, YANGA ZILIVYOPELEKA KILIO NA KUVURUGA TIMU ZA WAARABU….HAWAAMINI KABISA…

SIMBA, YANGA ZILIVYOPELEKA KILIO NA KUVURUGA TIMU ZA WAARABU….HAWAAMINI KABISA…

Habari za Michezo leo

Tangu mwaka 2014, walau timu moja kutoka Algeria au Morocco zilifanikiwa kuingia kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, lakini rekodi hiyo imeharibiwa na Simba na Yanga ambazo msimu huu zimekwamisha timu kutoka mataifa hayo kutinga robo fainali.

Simba iliizuia Wydad Casablanca iliyokuwa nayo kwenye kundi B, ambapo wote walikuwa na pointi tisa lakini Simba ikapita kwa faida ya matokeo bora ya ugenini pale timu hizo mbili zilipokutana. Simba ililala 1-0 kule Morocco lakini ikashinda 2-0 nyumbani Dar es Salaam.

Kwenye kundi lao tayari Asec Memosas ilishafuzu kwenda hatua ya robo fainali na ilitakiwa timu moja kati ya Simba, Wydad na Jwaneng Galaxy, lakini Simba ndio ilifuzu na kusababisha Morocco ishindwe kuingiza timu kwenye robo fainali kwani AS FAR ambayo ilishiriki ilitolewa kwenye hatua za awali.

Hiyo pia ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Wydad kutolewa kwenye hatua ya makundi katika mara zote ilizowahi kushiriki michuano hii na kufika hatua hiyo.

Kwa upande wa Yanga pia mambo yalikuwa ni hivyo hivyo. Iliizuia Algeria isiwe na timu hata moja kwenye robo fainali ya michuano hii baada ya kuiondosha CR Belouizdad.

Belouizdad na Yanga ambazo zote zilikuwa kundi D, zilimaliza kundi kwa alama nane lakini Yanga ilikaa juu ya Waarabu hao wa Algeria kwa sababu ilipata matokeo mazuri kwenye mechi zao mbili za makundi walipokutana. yanga ilipasuka 3-0 katika mechi ya ufunguzi wa Kundi D dhidi ya Belouizdad kule Algeria kabla ya kuja kuichakaza 4-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Baada ya kutoka kwa Belouizdad, Algeria ikaambulia patupu kwenye hatua ya robo fainali kwa sababu mshiriki mwingine kutoka nchi hiyo CF Constantine alitolewa kwenye hatua ya awali na Etoile du Sahel.

Yanga iliungana na Al Ahly ambayo ilimaliza kinara wa kundi D kwa pointi 12.

SOMA NA HII  OHOOO...YANGA MMEMSIKIA OKRAH HUKOO....BALAA LAKE MPAKA NABI ATAKUWA MWEKUNDU..