Home Habari za michezo KISA KUKOSEKANA KWA DIARA YANGA…MSHERY AWEKA REKODI HII YA KIBABBE CAF…MAMBO YAANZA...

KISA KUKOSEKANA KWA DIARA YANGA…MSHERY AWEKA REKODI HII YA KIBABBE CAF…MAMBO YAANZA KUWA MAZURI KWAKE…


Ndio. Golikipa wa Yanga Abutwalib Mshery,  ameweka rekodi ya kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa kwa ngazi ya klabu akianza kwenye mechi dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini, katika Ligi ya Mabingwa.

Mshery ndio amesimama kwenye milingoti mitatu akichukua nafasi ya Djigui Diarra ambaye hakuwepo kabisa kwenye kikosi cha jana.

Katika historia yake ya soka hii ndio itakuwa mara yake ya kwanza kucheza mechi ya kimataifa ya michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu.

Kwa msimu huu hii inakuwa ni mechi ya pili kwa Mshery, baada ya kufanya hivyo pia kwenye mechi dhidi ya Coastal Union ambayo iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0.

Kikosi cha Yanga kilichoanza  golikipa ni, Abdutwalib Mshery mabeki, Djuma Shaban, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto, viungo Yannick Bangala, Khalid Aucho, Feisal Salum, Dickson Ambundo, washambuliaji Fiston Mayele, Aziz Ki, Jesus Moloko.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA KULAMBA POSHO ZA KIMADRID WAKIBEBA UBINGWA WA CAF...KAZI INAANZA KESHO...