Home Habari za michezo UNAAMBIWA SIMBA WALICHEZA PIRA GIMBI DHIDI YA WYDAD MCHAMBUZI AFUNGUKA HAYA

UNAAMBIWA SIMBA WALICHEZA PIRA GIMBI DHIDI YA WYDAD MCHAMBUZI AFUNGUKA HAYA

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EA Radio, Ibra Kasuga amesema kuwa, Timu ya Simba haikucheza mchezo wowote mzuri kwenye mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca kama ambavyo baadhi ya watu wanavyosema.

Ibra amedai kuwa alichokiona kwenye mchezo huo uliopigwa weekend iliyopita nchini Morocco, ni ile ari ya wachezaji wa Simba kupambana na kuwa na hamu ya kupata matokeo lakini hakuna soka lolote la maajabu walilocheza.

“Watu wanaamini Simba alivyoheza dhidi ya Wydad ni kama alicheza vizuri lakini kwangu mimi Simba hakucheza mpira wowote mkubwa dhidi ya Wydad, ila kilichoonekana kwenye mchezo huo ni ile ari/morali.

“Yaani hakuna mpira wowote wa ajabu alioucheza Simba kwenye ile game isipokuwa tu kuna ile ari au utayari timu ilionekana kuchangamka.

“Yaani timu ilionekana angalu ile work-rate ule ufanyaji wao wa kazi uliongezeka uwanjani, unaona wachezaji wanakimbia, unaona wachezaji wanajaribu kufanya marking kwa haraka zaidi kitu ambacho hakikuwepo kwenye michezo ya nyuma,” amesema Ibra Kasuga.

SOMA NA HII  BOCCO NA SIMBA SASA NI MAJI YA JIONI WAKATI WOWOTE TUTASIKIA TANGAZO HILI