Home Habari za michezo GAMONDI AFUNGUKA KUHUSU MASTAA HAWA KUKOSA WAPINZANI KIKOSINI

GAMONDI AFUNGUKA KUHUSU MASTAA HAWA KUKOSA WAPINZANI KIKOSINI

Habari za Yanga SC

Wakati Yanga wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha wa Yanga ametoa kauli ya kuwajibu wale wote wanaojaribu kumshauri kikosi cha kupanga kuelekea mchjezo huo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Gamondi anasema;

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, tunawajua vizuri Mtibwa Sugar, ila kwa nyie Mnaotaka nicheze na mawinga niambieni namtoa nani ili wao wacheze, nimtoe Aziz Ki? Nimtoe Pacome? Nimtoe Clement? Binafsi naamini tunacheza mpira mzuri tukiwa na Viungo kuliko Mawinga” – amesema

Yanga wataikaribisha Mtibwa Sugar Disemba 16 katika Uwanja wa Chamazi.

SOMA NA HII  YANGA VS AZAM SIO POA KWA HALI HII LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA