Home Simba SC HII SIMBA YA MSIMU UJAO TEMA MATE CHINI AISEE..HUKU KUNA BANDA KULE...

HII SIMBA YA MSIMU UJAO TEMA MATE CHINI AISEE..HUKU KUNA BANDA KULE SAKHO..LITAKUFA JITUU


KAMBI ya Simba imenoga baada ya kiungo fundi wa mpya, Saido Kanoute akitua na kulimsha mapema pamoja na wenzake, usajili uliofanywa na mabosi wa klabu hiyo umeibua vita tano kikosini na kumpa kazi Kocha Didier Gomes, huku mastraika, John Bocco na Chris Mugalu wakilianzisha upyaaa.

Simba iliyojichimbia kambini mjini Rabat Morocco na juzi walikuwa uwanjani kuvaana na FAR Rabat inayonolewa na kocha wao wa zamani, Sven Vandenbroeck, imesajili wachezaji 12 wakiwamo wazawa na nyota wa kigeni kutoka nchi za Malawi, DR Congo, Senegal na Mali.

Kutua kwa wachezaji hao kumeibua vita mpya nne mbali na ile ya Bocco na Mugalu ambao msimu uliopita wakichuana vikali kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora hadi dakika za mwisho wa pambano lao la Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo waliowatungua mabao 4-0.

Vita hizo mpya zinahusisha nyota hao wapya waliosajiliwa hivi karibuni na wale waliokuwapo msimu uliopita.

Licha ya usajili wa kishindo ambao Simba imeufanya, ni nafasi sita ambazo wachezaji walioitumikia timu hiyo msimu uliomalizika wana uhakika wa kuendelea kucheza msimu ujao lakini zingine tano, benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha Didier Gomes litakuwa na kazi kubwa ya kuamua nani aanze kati ya wale waliosajiliwa kipindi hiki na wale waliokuwa wakizicheza msimu uliopita.

Nafasi hizo tano ni ile ya mshambuliaji wa kati, beki mmoja wa kati, kiungo mmoja wa ulinzi ma winga wa kulia na kushoto.

BOCCO NA MUGALU

Vita ya kuwania nafasi ya mshambuliaji wa kati, bila shaka itaendelea kuwahusisha Bocco na Mugalu ambao msimu uliopita benchi la ufundi la Simba lilikuwa likipendelea kuwatumia zaidi kulinganisha Meddie Kagere.

Mugalu alipata nafasi zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Bocco akipata nafasi zaidi ya kucheza katika Ligi Kuu.

Lakini kasi ya kufumania nyavu iliyoonyeshwa na Mugalu katika dakika za lala salama kwenye Ligi Kuu inaweza kumuweka katika wakati mgumu Bocco aliyeibuka kinara wa ufungaji baada ya kupachika mabao 16.

Kama sio bao la penalti alilofunga katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Namungo, Bocco angeweza kumaliza akiwa amefumania nyavu mara 15 sawa na Mugalu aliyemaliza akiwa nafasi ya pili.

WINGA MOTO

Lakini ukiondoa hao, kutakuwa na vita ya kuwania nafasi ya winga wa kushoto baina ya Ousmane Sakho, Duncan Nyoni na Hassan Dilunga.

Ushindani mkubwa katika vita hiyo unaweza kuwa baina ya Sakho aliyesajiliwa na Simba kutokea Teungueth ya Senegal na Nyoni aliyenaswa kutoka Silver Strikers ambao kila mmoja ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupiga chenga, kai, kupiga pasi za mwisho na kufunga mabao

SOMA NA HII  MZAMIRU ASHUSHA PRESHA SIMBA SC...

Ni kama ilivyo upande wa kulia ambako kutakuwa na vita baina ya Bernard Morrison aliyekuwmo Simba msimu uliopita na Peter Banda ambaye amenaswa na timu hiyo kutoka Nyasa Big Bullets ya Malawi ingawa pia kutakuwa na ushindani kutoka kwa Jimson Mwanuke na Yusuph Mhilu

KIUNGO CHA KATI

Vita ya nne ni ile ya kiungo mmoja wa ulinzi ikiwa kocha Gomes atatumia mfumo wa kucheza na wachezaji wawili katika nafasi hiyo.

Tayari Lwanga Taddeo anaonekana ataendelea kucheza katika nafasi mojawapo lakini nyingine itaibua ushindani baina ya Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na nyota mpya, Sadio Kanoute.

Kanoute na Mkude kila mmoja ana utulivu na uwezo mkubwa wa kuchezesha timu, umiliki wa mpira pamoja na kukaba hivyo mmojawapo anaweza kuwa na nafasi kubwa ya kuwemo katika kikosi cha kwanza.

BEKI YA KATI

Katika nafasi ya beki mmoja wa kati, Joash Onyango anaonekana hana presha kubwa lakini kwa mwenzake, Pascal Wawa aliyekuwa akicheza naye sambamba msimu uliopita atapaswa kufanya kazi ya ziada kurudi katika kikosi cha kwanza kutokana na usajili wa beki wa timu ya taifa ya DR Congo, Enock Ibanga ‘Varane’

Wakati Wawa akiwa na uwezo mkubwa wa kuchezesha timu kutokea nyuma na kutibua mipango ya wapinzani, Varane yeye ni fundi wa kukaba na kupora mipira kwa wapinzani pia ni mzuri hewani.

MSIKIE BOCCO

Nahodha wa Simba, John Bocco alisema kuwa anafurahi kuona kunakuwa na ushindani kwani utaifanya timu ifanye vizuri

“Naupongeza uongozi kwa kufanya usajili mzuri ambao naamini utakuwa chachu kwetu kutimiza malengo yaliyowekwa ambayo ni kutwaa makombe ya ndani na kufanya vizuri kimataifa.

Simba ni timu kubwa hivyo naamini kila mchezaji anajua wajibu wake kwa timu na suala la kucheza linabakia kwa mwalimu na benchi la ufundi ingawa naamini yeyote atakayepewa nafasi ataifanya timu ipate matokeo mazuri,” alisema Bocco, huku kocha wa zamani wa Ihefu, Maka Malwisi alisema mahitaji ya timu katika usajili huo ndio yataamua kucheza au kutocheza kwao

“Kuna sajili mbili tofauti hapo. Moja Ni usajili wa kuziba mapengo, wanaingia moja kwa moja ila kuna wale wa jicho la kocha kwa timu ya baadaye, hao wataingia taratibu sawa na mpango kazi wake kocha, hao ni kina Jimson, Mhilu. Ila hawa wa kimataifa sijajua nani ni mbadala wa kina Chama na Luis au ndio kama tulivyoambiwa na Crescentius Magori, wanafanya skauti ya muda mrefu haiendani na kuondoka kwa hao,” alisema.