Home Habari za michezo FAMILIA WAANIKA KILICHOMUUA BI HINDU….ALIKUWA AKIPUMULIA MASHINE NYUMBANI…”ALIKUWA NA WATU WENGI”…

FAMILIA WAANIKA KILICHOMUUA BI HINDU….ALIKUWA AKIPUMULIA MASHINE NYUMBANI…”ALIKUWA NA WATU WENGI”…


CHUMA Selemani maarufu kama Bi Hindu amefariki dunia asubuhi ya leo baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na kansa ya mapafu.

Baada ya muda mfupi kutokea kifo chake binti yake aliyejitambulisha kwa jina la Mwanadini na kuthibitisha ni kweli wamefiwa na mama yao mzazi.

Mwanadini amesema mama kifo cha mama yake kilimpata nyumbani kwake baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na kansa ya mapafu.

“Tulitoka hospital na kumuuguzia nyumbani ambapo alikuwa anapumulia mashine ‘Oxygen machine’ kwa ufupi Watanzania wafahamu hilo, tutaendelea kuwajulisha mengine kwa kadri tutakavyoweza”.amesema.

Mwanaidi amesema bado hawajapanga ratiba za mazishi hadi watakapokaa kikao cha ndugu kujua watazika lini na wapi.

“Kupitia nyinyi tunawaambia mashabiki wa mama yetu Bi Hindu kwamba msiba upo Magomeni mtaa wa Uweje, tutaendelea kuwapa taarifa nyingine kadri tutakavyopata maamuzi ya nini tufanye”. amesema Mwanadini na kuongeza;

“Mama alikuwa na watu wengi kuanzia kwenye kazi yake ya sanaa hadi kwenye upenzi wake na Simba, hivyo naamini wakipata taarifa hii watajumika nasi”.

Amesema watamkumbuka mama yao kwa upambanaji wake na kusimamia anachokiamini bila kujali Dunia inakaa kinyume naye.

SOMA NA HII  KISA SAFARI YA ZANZIBAR ALLY KAMWE AMPIGA KIJEMBE FEI TOTO