Home Habari za michezo UCHAGUZI MKUU YANGA: MANARA ATANGAZA ‘SAPRAIZI’ KUBWA KWA MASHABIKI….UKUMBI MZIMA WALIPUKA KWA...

UCHAGUZI MKUU YANGA: MANARA ATANGAZA ‘SAPRAIZI’ KUBWA KWA MASHABIKI….UKUMBI MZIMA WALIPUKA KWA SHANGWE….


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara ametangaza kwa wanachama wa klabu hiyo kwamba baada ya uchaguzi wa viongozi wao basi kutakuwa na sapraizi kubwa.

Manara ameyasema hayo wakati akisubili zoezi la kupiga kura lianze hali iliyofanya wanachama wa klabu ya Yanga kupiga shangwe.

Taarifa hiyo inachochea tetesi zinazoashilia wachezaji wao wapya akiwemo Aziz Ki kuja katika ukumbi huu wa mkutano wa uchaguzi.

Manara aliwageukia wagombea na kuwaambia mashabiki wa Yanga wanataka makombe na sio kitu kingine chochote.

“Nyie nendeni mkaijenge Yanga uwanjani, kiuchumi lakini wanachama wanataka makombe na sio kitu kingine kwani hiyo ndio furaha yao,” amesema Manara na kauli hiyo iliibua shangwe kutoka kwa wanachama.

UCHAGUZI KWA MATAWI

Baada ya Manara kumaliza kuzungumza alimkaribisha Mwenyekiti wa uchaguzi, Malangwe Ally Mchungahela.

Mchungahela aliwataka wanachama kupiga kura kwa kufuata utaratibu ambao walikubaliana.

“Kura mtapiga kwa matawi na tutaanza kuita moja moja, kanuni zingine za uchaguzi zizingatiwe.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA SIMBA VS MAZEMBE JUZI..SHABAN DJUMA AGUNA KISHA ATOA KAULI KUELEKEA GAME YA KESHO KUTWA