Home Habari za Yanga Leo YANGA YAWAFICHA CHAMA, AZIZ KI, BALEKE…WAHOFIA WAPINZANI

YANGA YAWAFICHA CHAMA, AZIZ KI, BALEKE…WAHOFIA WAPINZANI

Habari za Yanga Leo, Aziz KI

YANGA ni kama imeshtuka vile. Baada ya kuiona Simba ipo kambini Ismailia, Misri na kusikia Azam FC nayo imeondoka nchini kwenda Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao, nao fasta wameamua kufanya jambo.

Mabosi wa klabu hiyo wakishirikiana na kocha Miguel Gamondi, wameamua kuwaondoa mastaa wa timu hiyo akiwamo Jean Baleke, Clatous Chama na Prince Dube jijini Dar es Salaam na kuwapeleka nje ya nchi ili kujifua kabla ya kuja kuliamsha kwa msimu ujao wa mashindano wakianza na Ngao ya Jamii.

Kambi ya yanga ipo Kigamboni maeneo ya AVIC Town ambapo imepelekea baadhi ya watu kufika na kuona mazoezi ya timu hiyo, hali inayopelekea mbinu zao kuwafikia wapinzani wao kirahisi.

Hata uwepo wa Baleke katika klabu hiyo umejulikana baada ya picha zake kusambaa akifanya mazoezi na Yanga, lakini wao wenyewe baddo hawajamtambulisa rasmi.

Inaelezwa kwamba Yanga wamepanga kuweka kambi yao Avic Town kabla ya kusafiri na kwenda kushiriki mashindano waliyoalikwa Afrika Kusini.

Huko watacheza dhidi ya Kaizer Chief na klabu ya Bundasliga FC Augsburg ikiwa ni mechi za kirafiki.

Klabu ya Yanga hadi saa imetambulisha wachezaji wapya 5, ambapo Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Abubakar Khomeiny Mlinda mlango, na Kiungo Duke Abuya.

Pia kuna habari za kiungo wa timu hiyo Khaleed Aucho kutowasili Kambini hadi sasa, bado tunaendelea kutafuta taarifa kina kuhusu uwepo wake ndani ya Wananchi.

SOMA NA HII  BEKI HUYU WA SIMBA APANDISHA MIZUKA SUPER LEAGUE