Home Habari za michezo BIL 25 ZATENGWA KUMVUA YANGA UBINGWA WA NBC….MO DEWJI ATAJWA..ISHU NZIMA IKO...

BIL 25 ZATENGWA KUMVUA YANGA UBINGWA WA NBC….MO DEWJI ATAJWA..ISHU NZIMA IKO HIVI….

Habari za Yanga

Hatimaye uongozi wa Simba umeweka wazi bajeti ya msimu mpya wa fedha wa klabu hiyo wa mwaka 2023/24, wenye malengo ya kukusanya jumla ya Sh25 bilioni kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato, huku ikiutaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara unaoshikiliwa na wapinzani wao, Yanga.

Simba pia imetangaza faida ya Sh2 bilioni iliyopatikana kutokana na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23, baada ya kukusanya Sh15.9 bilioni, licha ya malengo waliyojiwekea ni kukusanya Sh13.6 bilioni ikiwa ni mapato ya klabu hiyo vyanzo mbalimbali.

Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, Mhasibu wa klabu Suleiman Kahumbu amesema “Matumizi ya 2022/23 yalipangwa kuwa Sh15,942,447,711 lakini tumeweza kutumia Sh15,936,829,943 tukabakiwa na balansi ya 5,617,768. Bajeti kwa mwaka 2023/2024 klabu imeweka malengo ya kukusanya Sh25,930,722,300 na imepanga kutumia kiasi cha Sh25,423,997,354, hivyo tutabaki na mapato ya ziada ya Sh506,724,946.”

“Aidha mapato yote hayo yanapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ndani ya timu hiyo kama fedha ya mdhamini, haki za matangazo, mapato ya mlangoni, uuzwaji wa jezi, wadhamini wadogo wadogo na kushiriki katika michuano ya AFL jambo ambalo limechangia kwa asilimia kubwa kupata mapato makubwa kwa klabu yetu msimu huu.

MO DEWJI ACHANGIA Sh2.4 BILIONI
“Katika bajeti ya fedha ya msimu wa 2022/23 Rais wa heshima wa Simba, Mohamed Dewji alituchangia Sh2.4 bilioni zilizoenda moja kwa moja kwenye kufanikisha kukusanya Sh15 bilioni ambazo zimetupa faida kwa kiasi kikubwa.”

USAJILI WATUMIA Sh2.3 BILIONI
“Kwenye usajili ambao tumeufanya msimu wa 2022/23 tuliweza kutumia Sh2.3 bilioni na ni kwa wale wachezaji wapya ambao tuliweza kuwasajili kwa wale wa kimataifa kwa manaa ya wachezaji wa nje na wandani.

MISHAHARA WATUMIA Sh4.8 BILIONI
“Mishahara wa wachezaji imetugharimu zaidi ya Sh4.8 bilioni, ikiwa ni bajeti ya msimu wetu wa fedha kwa mwaka 2022/23 hapa utaona ni kwa kiasi gani tunaweza kutumia fedha vizuri kuwalipa wachezaji wetu stahiki zao.

BONASI ZA WACHEZAJI Sh1.5 bilioni
“kwenye michezo ambayo Simba inacheza, kuna bonasi kwa ajili ya timu na hapa inakuwa kwa upande wa timu zote ile ya kiume na ile ya kike, Simba Queens,” amesema Mhasibu wa Simba, Suleima Kahumbu.

Katika mkutano huo ulianza saa 5:00 asubuhi uliofunguliwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amesema Simba imeshafanya mambo mengi makubwa, yaliyopita, yanayofanyika sasa na mengine yanakuja.

Amesema viongozi wenye dhamana ya kuongoza klabu hiyo wapo tayari kupokea maoni na kukosolewa ili kuipeleka Simba mbele na kufikia malengo yanayotarajiwa.

“Lengo letu ni kujenga umoja. Mfano mtu anasema uwekezaji hauna faida wakati kabla ya uwekezaji mapato yalikuwa Sh1.6 bilioni, mara baada ya uwekezaji yamepanda hadi Sh6.9 bilioni.

Afrika tulikuwa nafasi zaidi ya 80 kwenye ubora na sasa tupo nafasi ya saba. Tunataka ukosoaji wenye tija, Kama mnakumbuka mlichanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja, pesa ile ilitumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju na pesa zingine zilitumika kuimarisha kambi ya timu,” amesema Mangungu.

Ameeleza wanajenga Simba imara kwa kizazi cha sasa na baadae, kuendelea kuonyesha kushirikiana na anaimani watafanikiwa na kufikia kule kinachotarajiwa na wanachama wa klabu hiyo.

Kwa upande wa mwakilishi wa mgeni rasmi, Nicolas Mihayo akimwakilisha Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo nchini (BMT), amesema anawapongeza Simba kwa kufuata malekezo ambayo ilipewa kufanyia kazi katika mapendekezo ya marekebisho ya katiba.

“Hili ni jambo la mfano kwa timu zingine, kuzingatia yale yanayoagizwa na Serikali na hivi karibuni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Damas Ndumbaro amewaita Simba na kuwataka kufanyia kazi mambo kadhaa ya katiba yao na inawapongeza na inawatakia kila la kheri,” amesema Mihayo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Simba, Jaji mstaafu Thomas Mihayo, amewataka viongozi kuwasikiliza wanachama wao na kuyafanyia kazi ili kuifanya klabu hiyo inakuwa imara.

Amesema kulingana na mkutano huo viongozi na wanachama kutoruhusu migogoro ambayo inaenda kuathiri timu yao kwa kupata matokeo mabaya katika michezo na ni toafuti na timu zingine ambazo wanakuwa na migogoro na kuathiri wachezaji.

“Kutofautiana ni jambo la kawaida, jambo la msingi ni namna gani ya kutatua maana kuna mengine yanaweza kuwa kweli na mengine sio kweli na zikitokea tofauti zisiingie kwenye timu. Mtu yoyote asiyeitakia mema Simba huyo ni msaliti,” Mwenyekiti huyo wa baraza la Ushauri Simba.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula ameweka wazi malengo ya klabu ni kujenga timu imara yenye uwezo wa kushinda makombe, kujenga taasisi imara na endelevu ikiwemo kujenga chapa imara ndani na nje ya Tanzania.

“Kujenga misingi imara na yenye tija kwa wanachama na wapenzi, kujenga uwezo wa kifedha ili kufikia malengo, kuvutia wafanyakazi wenye weledi, kujenga misingi imara ya mawasiliano na matawi/wanachama.

Tumefanya maboresho makubwa kwenye benchi la ufundi tukianzia na kocha nadhani wote mnaona, idara ya afya ya timu yetu, tuna madaktari bora sana.

Pia tumeimarisha timu ya vijana kwa kutafuta vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini, timu yetu ya wanawake imekuwa bora sana. Eneo lingine ni tumeimarisha uhusiano kwa kiasi kikubwa na wadhamini wetu.

“Sehemu nyingine kubwa ni kushinda Ngao ya Jamii mbili kwa timu zetu za wanaume na wanawake kuwa mashabiki bora wa AFL. Simba ilileta Rais wa FIFA na kubwa zaidi kuitangaza Tanzania Kajula.”

Ameongeza wanataka kuwa mabingwa wa ndani na nje ya uwanja, walianzisha WhatsApp channel wakawa wanasemwa lakini leo wanaongoza kuwa namba moja Afrika Mashariki na Kati.

“Tutaendelea kujenga rasilimali za Simba na eneo lingine ni kuwa na wafanyakazi wenye weledi na uwezo mkubwa sana. Mbele tunaangalia kuboresha mapato, kuimarisha biashara ya jezi.

Sandaland amefanya yale mliyokuwa mnayataka kama jezi kutoka mapema na jezi yenye ubora, mzabuni aliyetimiza malengo yenu wanachama, Mwaka huu tunaangalia namna ya kushirikisha matawi katika uuzaji wa jezi ili kuwaongezea mapato,” amesema Kajula.

Ameeleza changamoto zilizopo upande wao ni rasilimali fedha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, kutanuka kwa mahitaji, kuumia kwa wachezaji, mabadiliko na ushindani kuongezeka na kuendelea kuwa timu namba moja.

SOMA NA HII  AUSSEMS: UBORA UTAIBEBA SIMBA SC KWA KAIZER