Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA SIMBA…MKWASA AINGIA UBARIDI…ADAI WATAKUWA WAMECHOKA MNOOO…

KUELEKEA MECHI NA SIMBA…MKWASA AINGIA UBARIDI…ADAI WATAKUWA WAMECHOKA MNOOO…


Kocha Mkuu Mkuu wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa ameonyesha wasiwasi wa kikosi chake kupambana kwa kiwango katika mchezo unaofuata dhidi ya Mabingwa watetezi Simba SC.

Ruvu Shooting itakua mgeni wa Simba SC Jumapili (Mei 08), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikikabiliwa na safari ya kuuwahi mchezo huo kutoka mkoani Kigoma ambako jana walicheza dhidi ya Young Africans, Uwanja wa Lake Tanganyika.

Kocha Mkwasa amesema atajitahidi kuwaweka sawa wachezaji wake kisaikolojia ili wapambane katika mchezo huo, licha ya ratiba kumkalia vibaya.

“Ni bahati mbaya kwangu na wachezaji wa Ruvu Shooting, tumepangwa kucheza na Namba Moja (Young Africans), mchezo unaofuata tutacheza na Namba Mbili (Simba SC), ukiangalia hapa kuna mtihani mkubwa, kibaya zaidi tutaanza safari ya kutoka Kigoma kurudi Dar es salaam, ratiba inaonyesha Jumapili (Mei 08) tutacheza mchezo wetu unaofuata, hivyo huenda ikawa nguvu kwa wachezaji wangu kucheza kwa nguvu kama ilivyokua hapa.”

“Naamini wachezaji wangu watakua na uchovu wa safari, lakini bado ninaami, watapmbana na ikiwezekana wataonyesha upinzani mkubwa dhidi ya Simba SC, japo nimetoa angalizo hilo la ukubwa wa safari inayotukabili kutoka hapa Kigoma hadi Dar es salaam.” amesema Mkwasa

Mchezo wa Duru la Kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara, Ruvu Shooting iliipeleka Simba SC Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kuambulia kichapo cha mabao 3-1.

SOMA NA HII  HITIMANA - YANGA WAKITAKA WATACHUKUA UBINGWA KWA NJIA ZOTE...SENZO ATIA 'UZITO' MABADILIKO...