Home news GAUCHO APEWA JEZI YA KAGERE MOROCCO

GAUCHO APEWA JEZI YA KAGERE MOROCCO


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika kikosi cha klabu ya Wanawake ya Chabab Atlas ya nchini Morocco, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ amekabidhiwa jezi namba 14.

Jezi hiyo hapa Tanzania imepata umaarufu mkubwa kwa kuvaliwa na Straika wa Simba, Meddie Kagere.

Gaucho amejiunga na Chabab akitokea kikosi cha klabu ya Simba Queens mwanzoni mwa mwezi Machi, mwaka huu.

Akiwa na Simba Queens alikuwa akivaa jezi namba 7, ambapo kumbukumbu ya mwisho akiwa na jezi hiyo ni kufunga bao kali la kideoni dhidi ya Watani zao wa Jadi Simba, katika ushindi wa mabao 3-0 Machi 5, mwaka huu.

SOMA NA HII  VALENCIA NA MAAJABU YAO KWENYE UWANJA ....MERIDIANBET WAFANYA JAMBO...