Home Habari za michezo SIMBA INAMTU HUYU MMOJA TU

SIMBA INAMTU HUYU MMOJA TU

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia East Africa Radio, Abissay Stephen amesema kuwa Klabu ya Soka ya Simba Sc ina mtu mmoja tu ambaye ni mpiga pasi mzuri kwenye eneo la kiungo.

Ngoma ambaye ni raia wa Congo DR amesajiliwa Simba SC msimu huu akitokea Al Hilal ya Sudan.

“Simba eneo la kiungo ambalo ni uti wa mgongo wa kucheza Lunyasi lina wachezaji mbao sio Passers wazuri (wapiga pasi wazuri), sasa hivi namwona Ngoma peke yake, sasa yule peke yake hawezi.

“Si huwa tunamuona anaingia kuna mechi ya juzi ameanza unamuona as a player very composed, anachukua mpira kwenye tight angle anageuka anaburuza mpira vizuri, anauomba anapewa anaburuza mpira vizuri, anaowapa wanafanya nini? wanageuka, wanakimbia, wanapokonywa, timu inaanza kukaba,” amesema Abissay Stephen.

SOMA NA HII  MBRAZIL SIMBA AWATUPA DONGO HILI ZITO YANGA...MAYELE ATUMA SALAMU MSIMBAZI