Home Uncategorized NAMNA METACHA MNATA ALIVYOTIBIWA KIDOLE CHAKE NA YULE MAMA MWENYE MIUJIZA

NAMNA METACHA MNATA ALIVYOTIBIWA KIDOLE CHAKE NA YULE MAMA MWENYE MIUJIZA


Nilielezea namna ambavyo nilicheza kwa wiki
mbili mfululizo huku kidole changu kikiwa
kimevunjika.


Sikuwa nimejua kama kidole kimevunjika lakini
muda wote wa wiki mbili nilicheza nikiwa na
maumivu makali kabisa. Niliendelea kuvumilia
kwa kuwa nilikuwa nina hamu ya kucheza mara
zote na kipindi hicho ndio nilikuwa nimeanza


kupata namba katika kikosi cha kwanza Mbao
FC chini ya kocha Ndayiragije.


Hisia zikawa kwamba kama nitakuwa
nimeumia, likija suala la kukaa nje, nitapoteza
nafasi na itakuwa kazi ngumu kuirejesha. Ndio
maana nikaendelea kupambana hivyohivyo na
maumivu.


Yaliponizidia, ndio nikaenda hospitali kupima na
wakasema natakiwa kupigwa X Ray, ikafanyika
hivyo ndio ikagundulika nimevunjika kidole
lakini wakasema tayari kilikuwa kimeanza
kuunga taratibu.


Nikawekewa hogo (POP) kwa wiki tatu lakini
hata baada ya hapo hakikuwa kimepona vizuri,


wakasema warudie kuweka hogo tena na safari
hii ilitakiwa kidole hicho kibanwe.


Sasa wakati huo ligi inakaribia kuanza,
nikakataa. Basi palepale mmoja wa makipa
wenzangu akaniambia kuna watu wanatibia
kidole kama hicho kwa asili. Yaani anakutibu
bila ya kukushika na unapona kabisa ndani ya
wiki mbili!


Basi nikawa natafakari, najiuliza hivi itakuwa
kweli! Akaniuliza kama amuite huyo mtu mara
moja aje ili aanze kunitibu, nikamuambia aache
kwanza niendelee kutafakari itakuwaje. Baada
ya muda kocha tuliyekuwa naye akaondoka na
pale Mbao FC akaja Flugence Novatus
(Mchezaji wa zamani wa Pamba).


Alipofika tu, nilimueleza tatizo langu kuhusiana
na kidogo namna ambavyo kilikuwa
kinanisumbua. Naye akaniambia vilevile, kuna
mama anatibu kwa wiki mbili tu unapona, tena
anakitibu bila ya kukigusa.


Safari hii kwa kuwa nilikuwa nimesikia mara ya
pili na huyu ni kocha, nikaamua kwenda. Kweli
yule mama wa Mwanza akaanza kunitibu,
nakwenda asubuhi na jioni, asubuhi na jioni
matibabu yanaendelea.


Kweli bila ya kukishika akawa ananitibu kila
kukicha, kama vile anazungusha mikono yake
hivi katika kidole. Kufika siku ya tatu,
akakifungua maana alikuwa amekifunga na
vijiti. Akafungua akaangalia akaanza kukunja
kukirudisha nyuma na mbele.


Alipoendelea kufanya hivyo, kweli kidole
kikaanza kwenda. Akanifunga tena akasema
itakuwa kwa siku mbili na itakuwa hivyo na
akifungua basi litakuwa suala la kukichua tu.


Basi mimi nikaona nimepata nafuu, nikafikiri
hivi; hakutakuwa na haja ya kukaa tena badala
yake ninaweza kuanza mazoezi angalau ya
kukimbia kuhakikisha nakuwa fiti kimwili.


Nikawa nakimbia naishia kwa yule mama,
anaendelea na matibabu yake ya kidole baada
ya hapo naondoka nakimbia tena kwenda
kumalizia mazoezi. Niliendelea hivyo kwa siku
tano, baada ya hapo kidole kikawa kimepona
kwa kiasi kikubwa na mazoezi ya kukunja na
kunyoosha yakaendelea kwa muda kidogo.


Kweli kidole hakikurudi katika ile hali yake
kabisakabisa, lakini ukweli kilipona na nikaweza
kurejea katika mazoezi ya kuanza kuucheza
mpira nikiwa nimepona kwangu kama kimiujiza
hivi kwa kuwa sikuwa nikiamini mwanzo na
sikuwa nimewahi kuona tiba ya aina hiyo.


Nilirejea mazoezini baada ya mwezi mmoja hivi
na wiki moja na ushee, nikawa fiti na
kufanikiwa kucheza mechi zote za mwisho


nikiwa Mbao FC na kweli nilicheza kwa kiwango
kizuri sana ikiwemo mechi moja dhidi ya Yanga
ambayo walitufunga kwa bao 1-0, nakumbuka
bao lilifungwa na (Thabani) Kamusoko.


Baada ya hapo wakaja watu wanasema
wananihitaji kwenda Yanga, nikawaambia nina
mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC,
wasubiri kwanza halafu ningependa kuwasikia
Azam pia wanasemaje.


Msimu ulipoishi nikaamua kurejea Azam FC,
nilipofika wakaniambia kwamba hawakuwa
wakinihitaji kwa kuwa hakuna nafasi.
Wakanitaka niendelee kupambana tu kwa kuwa
siku moja wanaamini ningerejea na kupata
nafasi pale. Nikalazimika kwenda Prisons ya
Mbeya tena kwa mkopo, niliomba mwenyewe


niende huko. Nakumbuka makipa walikuwa ni
Aaron Kalambo na mwingine Prosper.
Tukaendelea kuchuana na kweli Kalambo
alikuwa bora zaidi yangu na alikuwa kipa wa
timu ya taifa.


Niliendelea kujifua naye kila mara bila ya
kuchoka. Lakini baadaye nikaona hakukuwa na
mwendelezo mzuri ambao ningependa wa
maisha pale. Nikaamua kuwa litakuwa jambo
zuri kama nitatafuta njia sahihi nyingine kwa
ajili ya maisha yangu ingawa nilijua ili nirudi
Azam lazima nionekane.


Nakumbuka Prisons nilidaka mechi mbili tu,
lakini muda mchache baadaye nikaitwa timu ya
taifa chini ya miaka 23. Baada ya kutoka pale,
nikarudi nikawaomba Prisons niondoke ili
niende nikatafute maisha yangu upande
mwingine. Wenyewe wakasema hawakuwa na
kipa mwingine na walikuwa ndio wameingia
katika raundi ya pili na mimi nikaendelea
kusisitiza kwamba nilikuwa nataka kuondoka.


Wakasema kwamba walikuwa wamenipa fedha.
Nikasema haina shida mimi nitarudisha hiyo
fedha. Nikazungumza na Mbao FC kwa kuwa
walikuwa wanatamani nirudi na wananipenda
kule. Nikawaambia ila kuna deni kama vipi

walipe ili niweze kumaliza na Prisons.
SOMA NA HII  UNITED SASA WASHINDWE WENYEWE KWA KIUNGO WA KEIZER