Home Uncategorized NYOTA WAPYA WA YANGA WAWEKA REKODI YAO

NYOTA WAPYA WA YANGA WAWEKA REKODI YAO

 

Nyota wapya Yanga, Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko leo, Agosti 20 wamewasili rasmi ndani ya ardhi ya Tanzania.
Mapokezi ya nyota hao yameweka rekodi kwa mashabiki wengi wa Klabu ya Yanga kujitokeza kuwapokea.

Safari ilianzia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo huko shangwe lilikuwa la kutosha.

Kisha shangwe likatua mpaka makao makuu ya Yanga, mitaa ya Jangwani.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said alibebwa juu mithili ya mfalme kwa kuwa alihusika kwenye kukamilisha dili hilo.

Nyota hao wote wawili wamesaini dili la miaka miwili kuitumikia Klabu ya Yanga ambayo inaendelea kuboresha kikosi chake baada ya kuwaacha nyota wake 16.

Pia wote walikuwa wanakipiga ndani ya Klabu ya AS Vita ya Congo moja ya klabu kubwa nchini Congo.

Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga amesema kuwa lengo kubwa la Yanga ni kujenga klabu bora yenye ushindani na inayovutia.

SOMA NA HII  KIUNGO WA SIMBA ATIBUA DILI LA NYOTA WA RWANDA KUTUA YANGA