Home Habari za michezo ALIYEPEWA UBOSI WA KUSAKA VIPAJI SIMBA KAYEYUKA KIMYA KIMYA?….HAJAWAHI KUTIA MGUU…

ALIYEPEWA UBOSI WA KUSAKA VIPAJI SIMBA KAYEYUKA KIMYA KIMYA?….HAJAWAHI KUTIA MGUU…

Habari za Simba

Klabu ya Simba msimu huu kabla haujaanza, ilileta mkuu wa kitengo cha “scouting” kwa ajili ya kusaka wachezaji wenye vipaji watakaoihudumia Simba kwa viwango vya kimataifa.

Usajili wa Mkuu yule wa Scouting Mella Daalder, Niliwahi kusema kwamba, wachezaji wazuri wapo tu na viongozi wanawaona, ishu ni viongozi kuweka pesa nzuri kuweza kuwanasa wachezaji hao.

Mpaka Mells Daalder anapewa kitengo Simba maana yake kuna kazi aliwahi kufanya na Simba au Simba waliona uwezo wake wa kuleta wachezaji wazuri ndipo wakaamua kumpa dhamana ile.

Mkuu wa kitengo cha Scouting, tangu atangazwe kuwa kiongozi wa Simba SC , hajawahi kuonekana uwanjani mimi.

Siyo tu uwanjani Simba ikiwa inacheza hapana, hajawahi kuonekana hata kwenye mechi kama Tanzania Prison vs Geita Gold akiangalia vipaji vya kusajili, hii ni kama upigaji tu.

Yanga hawana Mkuu wa Scouting ila ndiyo Club hadi kufika sasa imenufaika na wachezaji wapya walioingia kwenye first eleven Yao, Maxi, Pacome, Kibabage na wengine, tofauti na Simba ni fabrice Ngoma na Che Malone pekee.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO....PAMBA FC WAIPIGA 'MKWARA WA KUFA NTU' SIMBA...WADAI LAZIMA 'LIFE JITU'...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here