Home Simba SC SIMBA YAMALIZANA NA BEKI KITASA MBADALA WA KAPOMBE

SIMBA YAMALIZANA NA BEKI KITASA MBADALA WA KAPOMBE


 ASILIMIA 90, Simba imemalizana rasmi na beki wa kulia wa AS Vita, Mkongomani Djuma Shaban na msimu ujao atavaa jezi zenye rangi ya nyeupe na nyekundu.

 

Beki huyo ni kati wachezaji walioipa ugumu Simba kupenya kwenye ngome ya Vita huku akisababisha mashambulizi kadhaa kwenye goli la wapinzani wake hao.


Mkongomani huyo alionyesha kiwango hicho katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Kinshansa, DR Congo ambao ulimalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 kwa njia ya penalti lililofungwa na Chris Mugalu.

 

Taarifa zimeeleza kuwa Simba imemalizana rasmi na beki huyo na msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi hicho. Mtoa taarifa huyo kilichobakia kwa beki huyo ni kusaini mkataba pekee baada ya klabu yake kutoa baraka ya kuja kujiunga na Simba.

 

Aliongeza kuwa beki huyo ambaye dau la usajili limefichwa alipendekezwa na kocha mkuu wa timu hiyo, Mfaransa Didier Gomes katika kukiimarisha kikosi chake katika msimu ujao.

 

“Katika kuiimarisha safu yetu ya ulinzi, benchi la ufundi limependekeza kumsajili beki wa kulia wa AS Vita, Djuma atakayekuja kusaidiana na Kapombe (Shomari).


“Viongozi tayari wamelikamilisha hilo kwa kuwafuata mabosi wa Vita kwa ajili ya kumalizana na kwa asilimia 90 limefanikiwa hilo baada ya kufikia muafaka mzuri wa kukubali kumuachia ili msimu ajiunge na timu.

 

“Kocha Gomes ndiye aliyependekeza usajili wake baada ya kuvutiwa naye katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tuliocheza DR Congo,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Anorld Kashembe kuzungumzia hilo alisema: “Muda wa usajili bado na hivi sasa timu ipo kwenye michuano ya mikubwa ya Afrika, hivyo ni ngumu kuzungumzia masuala ya usajili.


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  JEMEDARI SAID ALIAMSHA TENA KUHUSU SIMBA....AFUNGUKA A-Z JINSI HESHIMA YAKE ILIVYO...