Home Yanga SC MRUNDI WA YANGA ATAJA WACHEZAJI WAKE ALIOWASAJILI

MRUNDI WA YANGA ATAJA WACHEZAJI WAKE ALIOWASAJILI

 


CEDRIC Kaze, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga na kufutwa kazi Machi 7,2021 baada ya ubao kusoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga amesema kuwa alihusika kwenye usajili wa nyota watatu ndani ya Yanga.


Kaze ambaye ni raia wa Burundi aliibuka ndani ya Yanga kurithi mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye yeye aliongoza kwenye mechi tano na alishinda mechi nne na sare moja ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika usajili ambao anasema kuwa alipendekeza na kuweza kuwasajili wachezaji hao ni Saido Ntibanzokiza ambaye ni kiungo mshambuliaji, Fiston Abdulazack ambaye ni mshambuliaji hawa wote ni raia wa Burundi.

Kwa upande wa wazawa anasema kuwa alipendekeza usajili wa beki Dickson Job kutoka Mtibwa Sugar ili kuongeza nguvu kwenye ulinzi.

“Nilipendekeza wachezaji watatu ambao walisajiliwa ndani ya Yanga hao waliweza kuwa ndani ya kikosi ila haikuwa katika mapendekezo yangu kwa asilimia kubwa.

“Wengi niliwakuta kwenye kikosi hivyo niliendelea kupambana nao na kwenda nao katika hali ambayo nilikuwa nahitaji kwenda nao,”.

Kocha huyo ambaye alikiongoza kikosi kwenye jumla ya mechi 18 za Ligi Kuu Bara alishinda 10, sare 7 na alipoteza mechi moja kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union anaiacha timu ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 50.


SOMA NA HII  YANGA YAIPIGA BONGE MOJA YA MKWARA SIMBA, YALITAKA TAJI LA NGAO YA JAMII