Home Uncategorized SIMBA KUIFUATA LEO STAND UNITED SHINYANGA

SIMBA KUIFUATA LEO STAND UNITED SHINYANGA


KIKOSI cha Simba leo kinatarajia kuanza safari kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa kesho, Februari 25 Uwanja wa CCM Kambarage.

Jana, Febuari 23 kikosi kilitia timu Mwanza na kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Stand United ambao ni wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Shirikisho.

Simba ilitinga hatua hiyo baada ya kushinda mabao 2-1 mbele ya Mwadui FC  Uwanja wa Uhuru, Dar na bingwa mtetezi wa kombe hilo ni Azam FC.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila wanahitaji heshima.

SOMA NA HII  SABABU YA MBEYA CITY KUWA NAFASI YA 17 HII HAPA