Home news MBRAZILI WA MAKIPA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA ISHU YA DIARRA KUPIGWA BENCHI AFCON…AFUNGUKA...

MBRAZILI WA MAKIPA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA ISHU YA DIARRA KUPIGWA BENCHI AFCON…AFUNGUKA HAYA…


KOCHA wa Makipa wa Klabu ya Yanga, Milton Nienov ameweka wazi kuwa michuano ya AFCON 2021 inayoendelea kutimua vumbi huko nchini Cameroon inaweza kuwa na athari kubwa kwa Djigui Diarra. Nyota ambaye amepata wakati mgumu kwenye kupata nafasi ya kucheza mpaka timu hiyo inaondolewa katika mashindano hayo hatua ya 16 bora.

Licha ya kuwa Mlinda mlango namba moja wa Yanga, Diarra ameonekana kukumbwa na wakati mgumu akiwa na timu yake ya taifa. Ambapo muda mwingi amekuwa akiwekwa benchi pasipo kupata nafasi ya kucheza. Jambo ambalo limemuibua kocha mpya wa makipa wa klabu ya Yanga, Milton Nienov.

Ambapo Nienov amesema kuwa hali aliyokumbana nayo Diarra kwenye michuano ya AFCON 2021 ni hatarishi kwenye safari yake ya mpira wa miguu. Kwani anaamini kuwa kuwekwa benchi kwa nyota huyo kutampunguzia ufanisi kwenye utendaji kazi wake mpaka atakapokuja kurejea tena.

Kauli ya Milton Nienov imekuja mara baada ya kuzungumza na kunukuliwa katika tovuti ya Global Publishers Januari 25, 2021 akikiri kuwa Diarra ni mlinda mlango bora kwenye ligi kuu ya NBC. Huku akikiri kuwa analitambua hilo toka akiwa kama kocha wa Makipa wa Simba.

“Nilikuwa nikimtazama Diarra wakati nikiwa na Simba, naweza kusema huyu ni miongoni mwa makipa bora zaidi ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa sasa na hili linathibitishwa na kuitwa kwake kwenye kikosi cha timu ya Taifa kubwa kama Mali,” alisema Nienov.

Milton aliongeza kuwa Diarra kukosa namba akiwa na timu yake ya taifa si jambo jema. Kwani jambo hilo linahatarisha ubora wa mchezaji huyo kwa kuwa anahitaji kucheza ndiyo aendelee kuwa kwenye ubora wake japokuwa hawawezi kuthibitisha moja kwa moja kuwa atarejea akiwa na kiwango cha chini. Hivyo basi wanasubiri arejee klabuni kwanza.

“Najua hajapata nafasi ya kucheza kutokana ushindani mkubwa wa namba anaokutana nao kwenye kikosi hicho na kwa upande wetu hilo sio jambo jema. Tunatamani kuona anacheza kwa sababu mara zote mchezaji anakuwa bora zaidi kadiri anavyopata nafasi ya kucheza. Kukaa benchi kunaweza hatarisha kiwango chake japokuwa hatuwezi kuthibitisha hilo kwa sasa mpaka atakaporejea,” alisema Nienov.

SOMA NA HII  KUHUSU MKUDE KUTUA SINGIDA....PLUIJM AIBUKA NA HAYA MAPYA....MBRAZILI SIMBA ATOA MSIMAMO...